ANKARA,UTURUKI
TIMU kutoka Tanzania ya watu wenye ulemavu Tembo Warriors ambayo ilifuzu kucheza mashindano hayo imeibuka na ushindi dhidi ya Uzbekistan kwa goli 2-0 kwenye mechi iliyochezwa leo Oktoba 3, 2022 nchini Uturuki.
Kwa matokeo hayo Tanzania inasubiri mchezo kati ya Poland na Hispania utakaochezwa majira ya saa 12:00 jioni, huo ndio mchezo utakaoamua nani kati ya Poland na Tanzania kushika nafasi ya pili katika kundi lao.
Shamrashamra za ufunguzi wa kombe hilo zimefanyika katika uwanja wa Ulker uliopo nchini Uturuki Septemba 30, 2022.

Mechi ya kwanza ya ufunguzin ilichezwa dhidi ya Uhispania Oktoba mosi, 2022 majira ya saa 7:00 mchana.
Katika mechi ya ufunguzi wenyeji Uturuki walishinda jumla ya mabao 3-0 dhidi ya Ufaransa




Discussion about this post