• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Serikali yawaonya Wakadiriaji Thamani za Ardhi na Mali

by bajeti
October 21, 2022
in Habari
0
Serikali yawaonya Wakadiriaji Thamani za Ardhi na Mali

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anjelina Mabula

Share on FacebookShare on Twitter

NA MIRIAM SARAKIKYA,ARUSHA.

WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anjelina Mabula amesema Serikali  itawachukulia hatua za kinidhamu   wathamini  wote watakaobainika kukiuka maadili ya taaluma zao.

Waziri Mabula ametoa kauli hiyo Oktoba 20,2022 mkoani Arusha wakati akifungua Mkutano Mkuu wa tatu wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Thamani wenye kauli mbiu isemayo ‘uthamini kichocheo cha uwekezaji’

Mabula amesema wapo wathamini wachache wanao chafua taaluma hiyo hivyo serikali inahitaji kufanya kazi na wafanyakazi waadilifu na wenye kusaidia kuleta maendele ya nchi na mtu mmoja mmoja

Aidha amefafanua kuwa Wakadiriaji wa Thamani za Ardhi na Mali wanatakiwa kufanya vizuri katika kazi zao kwani wasipofanya hivyo watasababisha hasara ya kutofikiwa kwa  malengo ya  mwekezaji mmoja mmoja,  taasisi na Taifa kwa ujumla na  kuitaka Bodi ya Usajili wa Thamani nchini kutambua thamani za Ardhi katika maeneo mbali mbali nchini .

Naye  Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wathamini nchini Cletus Ndjovu amebainisha kuwa tayari bodi hiyo imeshamchukulia hatua mmoja wa wathamini

“Kutokana na utovu wa nidhamu Mthamini mmoja amefungiwa  huku   kampuni za usajili tano  zimepigwa faini kwa viwango mbalimbali na wathamini watatu wamepewa onyo”ameeleza Ndjovu

Next Post
Masanja:Onesho la SITE kufungua fursa ya Utalii Dar es Salaam

Masanja:Onesho la SITE kufungua fursa ya Utalii Dar es Salaam

Taasisi ya Jai yaomba gharama za matibabu ya figo kupunguzwa

Taasisi ya Jai yaomba gharama za matibabu ya figo kupunguzwa

Dkt.Mpango:Serikali inatambua umuhimu wa sekta binafsi

Dkt.Mpango:Serikali inatambua umuhimu wa sekta binafsi

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In