• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Dkt.Mpango:Serikali inatambua umuhimu wa sekta binafsi

by bajeti
October 23, 2022
in Habari
0
Dkt.Mpango:Serikali inatambua umuhimu wa sekta binafsi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akipokea kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kuwa hifadhi bora zaidi barani Afrika ya mwaka 2022 jijini Dar es Salaam Oktoba 22,2022, inayotolewa na World Travel Award. Kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

MAKAMU  wa Rais Dkt. Philip Mpango amesema Serikali inatambua umuhimu wa sekta binafsi kama kichocheo cha kuimarisha sekta ya utalii hapa nchini hivyo imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kuleta mageuzi  hususani katika  sheria na maboresho ya sera ya bajeti ili kusaidia ukuaji wa sekta hiyo.

Makamu wa Rais amesema hayo 22 Oktoba 2022, wakati wa ufunguzi wa onesho la sita la kimataifa la utalii la Swahili (Swahili International Tourism Expo) linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.

Aidha ametaja hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali ikiwemo kuboresha miundombinu ya huduma za utalii ambayo ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa ya mwendokasi, kujenga na kukarabati barabara, viwanja vya ndege, kambi za watalii na kuongeza kasi ya Shirika la Ndege la Taifa ili kurahisisha safari za ndani ya Tanzania pia.

Amesema Utalii ni miongoni mwa sekta zinazopewa kipaumbele na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye  amekuwa bingwa wa kuimarisha sekta hiyo baada ya Uviko-19, kupitia makala ya ubunifu ya The Royal Tour ambayo imepelekea matokeo chanya ya kuongezeka kwa watalii na mapato nchini.

Hata hivyo Dkt.Mpango ametoa wito kwa wawekezaji kuchangamkia fursa kubwa na ambazo hazijatumika hasa katika sekta ya utalii kutokana na Tanzania kutoa mazingira mazuri ya amani na utulivu kwa biashara na uwekezaji.

Aidha  amewahimiza wawekezaji wote watarajiwa pamoja na washiriki wote wa onesho hilo kutumia maonesho hayo kama jukwaa la kupanua biashara na kuimarisha ushirikiano ili kuipeleka sekta ya katika viwango vipya na vya juu zaidi.

Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt.Pindi Chana amesema Wizara hiyo imeweka malengo ya kuongeza watalii wasiopungua milioni 5 pamoja na kuongeza  pato la taifa la dola bilioni 6 ifikapo mwaka 2025.

Aidha ameongeza kuwa Wizara imeendelea na jitihada kutangaza vivutio hususani katika ukanda wa Kusini mwa Tanzania na kuwakaribisha wawekezaji na wadau wa utalii kuwekeza katika maeneo hayo.

Awali Waziri wa Utalii na Mambokale wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Simai Mohammed Said amesema ipo haja ya kuongeza jitihada na kuwekeza katika utalii wa urithi ikiwemo kufanya tafiti na kuhifadhi maeneo ya urithi yatakayopatikana kupitia tafiti hizo.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango (aliyenyanyua mkono)akifurahia ngoma za asili wakati alipowasili katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City Jijini Dar es salaam Oktoba 22,2022 kwa ajili ya ufunguzi wa Onesho la Sita la Kimataifa la Utalii la Swahili (SITE).Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Katika ufunguzi wa Maonesho hayo, Shirikisho la Chama cha waongoza watalii nchini wametoa zawadi ya kumtambua Rais Samia Suluhu Hassan kama muongozaji bora wa Watalii kwa mwaka 2022.

Onesho la Kimataifa la Utalii la Swahili kwa mwaka 2022 linahudhuriwa na washiriki zaidi ya 200 kutoka ndani na nje ya Tanzania, zaidi ya wanunuzi 100 wa kimataifa kutoka ndani na nje ya Afrika pamoja na wageni wa kibiashara 5,000 ambalo  lilianzishwa mwaka 2014 kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana hapa nchini pamoja na fursa za uwekezaji.

 

Next Post
Halmashauri zatakiwa kuipa kipaumbele miradi ya mazingira

Halmashauri zatakiwa kuipa kipaumbele miradi ya mazingira

AMREF yatoa Dola Milioni 1.9 kuimarisha mifumo ya afya  Afrika

AMREF yatoa Dola Milioni 1.9 kuimarisha mifumo ya afya Afrika

TAWA:Uharibifu wa mazingira unasababisha wanyamapori kukosa mwelekeo

TAWA:Uharibifu wa mazingira unasababisha wanyamapori kukosa mwelekeo

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In