• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Halmashauri zatakiwa kuipa kipaumbele miradi ya mazingira

by bajeti
October 24, 2022
in Mazingira
0
Halmashauri zatakiwa kuipa kipaumbele miradi ya mazingira

Mtambo wa kuchimba visima virefu ukiendelea na kazi katika kijiji cha Bulende wilayani Nzega Mkoa w Tabora ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo yenye Ukame nchini (LDFS) (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,TABORA

 

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Switbert Mkama amezitaka halmashauri nchini kuipa kipaumbele miradi ya mazingira ili kusaidia  kurejesha Ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula.

Haya hivyo Dkt.Mkama ameonesha kutoridhishwa na usimamizi wa Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula unaotekelezwa katika Halmashauri ya Nzega mkoani Tabora licha ya kuwa tayari fedha zimeshatolewa na Serikali kwa Halmashauri za wilaya zinazotekeleza miradi hiyo.

Dkt.Mkama ametoa kauli hiyo Oktoba 24,2022 wilayani Nzega Mkoa wa Tabora  wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo yenye Ukame nchini (LDFS).

Amesema inashangaza kuona namna wilaya inavyotekeleza miradi ya Serikali kwa kutoipatia kipaumbele miradi ya mazingira kama inavyofanya kwa miradi mingine katika wilaya hiyo.

“Matumizi ya fedha katika mradi huu hayaridhishi hata kidogo, kwa mwaka 2022/23 Nzega mmetengewa Sh. Bilioni 2.3 na kati ya hizo Sh.Milioni 467.6 zipo kwenye akaunti bado hazijatumika na mpaka Desemba zinatakiwa ziwe zimetumika hali hii hairidhishi hata kidogo,” amesema Dkt.Mkama

Dkt.Mkama aliutaka uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega kujitathmini kuhusu utendaji wake na kutoa siku saba wa kuandaa mpango kazi wa utekelezaji wa kazi hiyo.

“Haiwezekani katika miezi miwili ya mkataba mkandarasi ana siku 23 hajafanya kazi yoyote lakini halmashauri iko kimya, mkurugenzi yuko kimya, mratibu wa mradi wa wilaya yuko kimya hamchukui hatua,” ameongeza Dkt.Mkama

Kutokana na hali hiyo alielekeza kusitishwa kwa mkataba dhidi ya mkandarasi huyo kwani ameshindwa kutekeleza majukumu yake na kuusimamia mkataba wake na halmashauri.

Aidha, katika hatua nyingine alimtaka Mkurugenzi wa halmashauri kumchukulia hatua Afisa Manunuzi kwa kufanya mchakato wa kununua mashine ya kukoboa mpunga kupitia mradi huo ambayo inadaiwa kutokidhi viwango na kutoendana na bei halisi.

Naibu Katibu Mkuu Mkama amebainisha kuwa  mashine hiyo inaoekana imetajwa kununuliwa kwa Sh. Milioni 50 tofauti na viwango na kuelekeza Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Ndani wa Serikali ishirikishwe na kupewa kazi ya kuikagua kujua kama inakidhi viwango.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Switbert Mkama (mwenye miwani) akikagua mashine ya kusaga nafaka iliyonunuliwa na kupitia Mradi wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula katika Maeneo yenye Ukame nchini (LDFS) wakati alipofanya ziara ya kukagua mradi huo wilayani Nzega Mkoa wa Tabora Oktoba 24,2022(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira)

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Nzega Evance Chambo amesema amepokea maelekezo hayo na kuahidi kuwa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya itasimamia kikamilifu utekelezaji.

Amesema atamuelekeza mratibu wa mradi wa wilaya awe anatoa taarifa za utekelezaji kila wiki ili kuhakikisha unatekelezwa kama ulivyopanga kuepuka changamoto kama hizo.

Dkt. Mkama na timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais amefanya ziara ya kutembelea na kukagua mradi wa LDFS katika wilaya za Magu (Mwanza), Nzega (Tabora) na Mkalama (Singida) na miradi mingine ikiwemo uchimbaji wa visima virefu vya maji katika kijiji cha Bulende na Bulambukana mradi wa ufugaji nyuki katika kijiji cha Lyamalangwa

 

Next Post
AMREF yatoa Dola Milioni 1.9 kuimarisha mifumo ya afya  Afrika

AMREF yatoa Dola Milioni 1.9 kuimarisha mifumo ya afya Afrika

TAWA:Uharibifu wa mazingira unasababisha wanyamapori kukosa mwelekeo

TAWA:Uharibifu wa mazingira unasababisha wanyamapori kukosa mwelekeo

NCCR-Mageuzi:Katiba Mpya ni hitaji la watanzania wote na si la chama kimoja

NCCR-Mageuzi:Katiba Mpya ni hitaji la watanzania wote na si la chama kimoja

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:6
  • Today's page views 6
  • Total visitors 13,062
  • Total page views 14,807

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In