• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

AMREF yatoa Dola Milioni 1.9 kuimarisha mifumo ya afya Afrika

by bajeti
October 25, 2022
in Habari
0
AMREF yatoa Dola Milioni 1.9 kuimarisha mifumo ya afya  Afrika
Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

SHIRIKA la Kimataifa la Amref Health Africa limetoa kiasi cha dola za kimarekani Milioni 1.9 kwa nchi nne za Afrika ili kuimarisha mifumo ya afya katika ngazi ya wilaya. Lengo la kutolewa kwa fedha hizo ni kusaidia mipango ya kuimarisha mifumo ya afya katika ngazi ya wilaya kote katika nchi nne za Afrika ikiwemo Tanzania, Uganda, Kenya na Malawi

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Shirika la Global Health Strategies kwa niaba ya AMREF iliyotolewa leo Oktoba 25,2022 jijini Nairobi,Kenya imeeleza kuwa  Shirika hilo litakabidhi Dola za Marekani Milioni 1.9 kama ruzuku ndogo kwa mashirika tisa ya Kiafrika yasiyo ya kiserikali.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa Mashirika yasiyo ya kiserikali yatashirikiana na Amref kutekeleza mikakati ya ndani ya kuboresha utoaji wa Chanjo dhidi ya Ugonjwa wa UVIKO-19 miongoni mwa watu walio katika hatari kubwa hadi mwisho wa 2023.

“Maendeleo haya yanatokana na majadiliano yaliyoongozwa na Mtandao wa Chanjo (VAN), mpango wa kujifunza kati ya viongozi wa afya katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ili kuboresha kampeni za chanjo nchini kote na kuongeza upokeaji wa Chanjo dhidi ya UVIKO-19”ilieleza taarifa hiyo.

Akizungumzia kuhusu fedha hizo,Meneja wa Mradi, Kitengo cha Usalama wa Afya Ulimwenguni katika Amref Health Africa Jackson Musembi alisema fedha hizo ni sharti watafute njia za kuongeza juhudi za kupambana na ugonjwa huo huku wakijenga upya kinga zao dhidi ya magonjwa mengine ya kuambukiza kupitia kuimarisha mifumo ya afya katika viwango vyote.

“Kupitia VAN, washirika wengine walio Afrika Mashariki na Kusini wanafanya kazi katika mipaka yote ili kushiriki mikakati iliyotayari kutumika kwa ajili ya utoaji ujumbe na uwasilishaji wake kwa ufanisi,tunajivunia kutoa msaada huu pamoja na washirika wetu kutoka kwa wakfu wa The Rockefeller Foundation.”alisema Musembi

Amref Health Africa ni Shirika la Kimataifa la Kiafrika lililoanzishwa mwaka wa 1957 na Madaktari wa Afrika Mashariki ili kutoa msaada muhimu wa matibabu kwa jamii za mbali za Afrika Mashariki.

Shirika hilo lenye Makao Makuu yake nchini Kenya, ndilo Shirika kubwa zaidi la Kimataifa lisilo la Kiserikali (INGO) lenye makao yake barani Afrika likiwa na lengo la kuongeza ufikiaji endelevu wa afya.

Amref inaendesha mipango mbalimbali katika nchi 35 barani Afrika, ikiwa imejifunza mambo kwa zaidi ya miaka 60 na kushirikisha Serikali, Jumuiya na Washirika.

Kadhalika, Amref Health Africa inashiriki katika uandaaji wa mipango(programu), uchangishaji, ushirikiano, utetezi, ufuatiliaji na utathmini ambapo pia  ina ofisi zake barani Ulaya na Amerika Kaskazini.

Next Post
TAWA:Uharibifu wa mazingira unasababisha wanyamapori kukosa mwelekeo

TAWA:Uharibifu wa mazingira unasababisha wanyamapori kukosa mwelekeo

NCCR-Mageuzi:Katiba Mpya ni hitaji la watanzania wote na si la chama kimoja

NCCR-Mageuzi:Katiba Mpya ni hitaji la watanzania wote na si la chama kimoja

Taasisi ya Jai kuendelea kusaidia jamii

Taasisi ya Jai kuendelea kusaidia jamii

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In