• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Taasisi ya Jai yaomba gharama za matibabu ya figo kupunguzwa

by bajeti
October 23, 2022
in Habari
0
Taasisi ya Jai yaomba gharama za matibabu ya figo kupunguzwa

Mwenyekiti wa Taasisi ya Jai na Diwani Mstaafu wa Kata ya Ukonga jijini Dar es Salaam Juma Mwaipopo (kulia) akizungumza na wanawake wa Mtaa wa Pugu Kinyamwezi Oktoba 22,2023 mara ya kutembelea kikundi chao.(Picha na mpigapicha wetu)

Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

MWENYEKITI wa Taasisi  isiyo ya kiserikali ya Jai Juma Mwipopo ameitaka Serikali kuangalia gharama za matibabu ya figo ili kusaidia watu wenye kipato cha chini kupata huduma hiyo.

Mwaipopo ambaye ni Diwani Mstaafu wa Kata ya Ukonga kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ametoa wito huo baada ya kutembelea wajane,wagonjwa na wazee wakiwemo wasiojiweza  katika maeneo mbalimbali ya Kata hiyo kwa lengo la kuwapatia misaada ili kujikimu na hali ya maisha

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Oktoba 23,2022 wakati wa ziara ya kutembelea wagonjwa katika Kata ya Ukonga, Mwaipopo amesema ni muhimu kwa  Seikali na wadau wengine wa Sekta ya Afya nchini kuangalia na kusaidia kupunguzwa kwa gharama za matibabu ya ugonjwa wa figo ili kusaidia kundi la watu wasio na uwezo kumudu gharama hizo.

“Nipo hapa leo nipo Mtaa wa Sabasaba na Kichangani nikiwa na mmoja wa wagonjwa wanaougua figo na  matatizo makubwa ya  mjane huyu ni kushindwa kupata matibabu  ya  figo kwa wakati.

“Mama akiwa anaumwa figo mwaka wa tatu sasa akiwa kitandani na tumbo limejaa hana msaada,anashindwa hata kuongea anatakiwa kwa wiki akatolewe maji mara tatu.

“Kila akienda hospitali kupata huduma hiyo lazima awe na Sh .120,000 hivyo kwa wiki anatakiwa awe na zaidi ya Sh.300,000 hali ambayo hawezi kuimudu,lakini kama kungekuwa na ufadhili au matibabu kuwa na gharama ya chini ya ndugu wangesaidia lakini haiwezekani kila wiki awe na fedha hizo”amesema Mwaipopo

Mwaipopo amebainisha kuwa mama huyo ikiwa hajapata matibabu kwa wakati, tumbo huvimba hali inayokatisha tamaa kwa familia hasa kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu.

“Kwa kweli kama hujaona huwezi kuwa na uchungu lakini inawezekana kuna wagonjwa wengi wa figo wako nyumbani kwa kushindwa kugharamia matibabu ya figo hivyo kupoteza maisha lakini kama serikali iliangalie jambo hili maana gharama ni kubwa sana”ameongeza Mwaipopo

Mwaipopo amekuwa akitembelea mitaa mbalimbali ya Kata hiyo na kutoa misaada mbalimbali vikiwemo vyakula na kusaidia watu wasiojiweza na wale wanaokabiliwa na magonjwa yenye gharama kubwa  ili kuwatia moyo na kuchangia gharama zao.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Jai na Diwani Mstaafu wa Kata ya Ukonga jijini Dar es Salaam Juma Mwaipopo akiwa na wanawake wa Kata ya Pugu Kinyamwezi jana mara baada ya kutembelea kikundi chao na kuwapatia msaada(Picha na Goodluck Hongo)

 

Next Post
Dkt.Mpango:Serikali inatambua umuhimu wa sekta binafsi

Dkt.Mpango:Serikali inatambua umuhimu wa sekta binafsi

Halmashauri zatakiwa kuipa kipaumbele miradi ya mazingira

Halmashauri zatakiwa kuipa kipaumbele miradi ya mazingira

AMREF yatoa Dola Milioni 1.9 kuimarisha mifumo ya afya  Afrika

AMREF yatoa Dola Milioni 1.9 kuimarisha mifumo ya afya Afrika

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In