NAIROBI,KENYA
MAMIA ya wanyamapori, wakiwemo Tembo na Pundamilia wamekufa katika mbuga za hifadhi nchini Kenya kutokana na ukame mbaya kabisa unaoukumba Ukanda wa Mashariki mwa Afrika.
Ripoti iliyotolewa Novemba 4,2022 na Shirika la Mbuga za Wanyama nchini Kenya (KWS) pamoja na taasisi nyingine wamehesabu Tembo 205, Nyumbu 512, Pundamilia 381 pamoja na Nyati 51 waliokufa kwa njaa na kukosa maji katika kipindi cha miezi tisa iliyopita.
Orodha ya wanyama waliokufa inajumuisha pia aina adimu ya pundamilia wapatao 49 na twiga 12.
Sehemu kadhaa za Kenya zimekabiliwa na misimu minne ya uhaba wa mvua, ambayo imeathiri vibaya maisha ya watu na ya wanyama, wakiwemo wafugwao na wale wa mwituni.
Mbuga za Kenya zilizoathiriwa zaidi na ukame ni Amboseli, Tsavo na mfumo anaui wa Laikipia-Samburu.




Discussion about this post