• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Serikali yaandaa Mkakati wa Kitaifa kuhusu Nishati Jadidifu

by bajeti
November 15, 2022
in Mazingira
0
Serikali yaandaa Mkakati wa Kitaifa kuhusu Nishati Jadidifu

Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati Emilian Nyanda,akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Novemba 10,2022 juu ya Nishati Jadidifu wakati wa warsha ya kuwajengea uwezo iliyoandaliwa na Taasisi ya Kuendeleza Nishati Endelevu na Uhifadhi wa Mazingira Tanzania(TaTEDO).(Picha na Goodluck Hongo)

Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

SERIKALI ipo katika maandalizi ya kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Jadidifu ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Mkakati huo wa Serikali umetangazwa Novemba 10,2020 jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati  Emilian Nyanda, katika warsha ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari iliyoandaliwa na Taasisi ya Kuendeleza Nishati Endelevu na Uhifadhi wa Mazingira Tanzania(TaTEDO).

Amesema Serikali imeandaa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Jadidifu kupitia Wizara ya Nishati ili kuongeza mchango wa Nishati Jadidifu katika upatikanaji wa nishati ya umeme nchini.

Amesema Nishati Jadidifu ni vyanzo vya kuzalisha umeme  visivyoisha ikiwemo  Upepo,Jua,Jotoardhi,Mawimbi ya bahari,Maporomoko ya maji ambayo ni chini ya megawati 10 na vingine ambavyo vinauwezo wa kuzalisha nishati bila kuchafua mazingira

“Serikali kupitia Sera yake ya Taifa ya Nishati ya mwaka 2015 inaweka kipaumbele katika uendelezaji wa rasilimali za nishati jadidifu kwa kuwa ni rasilimali endelevu na nyingi zinapatikana hapa nchini.

“Katika Sekta ya Nishati ukitaka upunguze athari za mabadiliko ya tabia nchi ni lazima utumie nishati jadidifu na matumizi bora ya nishati.

“Sera yetu inatambua nishati jadidifu lakini na sera zingine kama ya Mazingira ya Mwaka 2021 na Mkakati wa Kitaita wa Mazingira ambazo zote hizo ni muendelezo wa nishati jadidifu”amesema Nyanda

Nyanda amebainisha kuwa kukamilika kwa mkakati huo kutatoa muongozo mzuri wa uendelezaji wa nishati jadidifu hapa nchini.

“Kwa sasa Wizara ya Nishati inaandaa Mkakati wa Kitaifa wa Nishati Jadidifu na tupo katika hatua nzuri na tayari mshauri elekezi ameshaanza maandalizi ya mkakati na kwa sasa anaendelea kupata maoni ya wadau hadi mwakani mwezi wa pili itakuwa imekamilika.

“Waandishi wa habari mtusaidie utoaji wa elimu ya umuhimu wa hii rasilimali ya Nishati Jadidifu ili wananchi wetu wajue jinsi serkali yao ilivyojipanga kuendeleza nishati hizo.

“Changamoto nyingine iliyokuwepo ni Sera ya Mkakati wa Nishati Jadidifu na jinsi gani unapata nyenzo ya kutekeleza sera yako inayotambua nishati Jadidifu ndio maana sasa hivi serikali imewekeza katika kuandaa Mkakati ya Nishati Jadidifu na Mkakati wa Matumizi Bora ya Nishati”amefafanua Nyanda

Hata hivyo Nyanda ameongeza kuwa mbali na mkakati hio lakini pia wanaandaa Mkakati wa Matumizi Bora  ya Nishati ili viende pamoja na Sera ya Mkakati wa Nishati Jadidifu.

Mratibu wa Mabadiliko ya Tabianchi na Tungamotaka kutoka Taasisi ya Kuendeleza Nishati Endelevu na Uhifadhi wa Mazingira Tanzania(TaTEDO) Shima Sago (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Novemba 10,2022 kuhusu umuhimu wa Nishatin Jadidifu.(Picha na Goodluck Hongo)

Kwa upande wake Mratibu wa Mabadiliko ya Tabianchi  na Tungamotaka kutoka TaTEDO Shima Sago amesema wanazungumzia Nishati Jadidifu hasa wakati huu kutokana na kwamba nishati zingine zinachangia uharibifu wa tabaka la juu linazozuia mionzi ya jua kufika ardhini hivyo kusababisha ongezeko la joto na ukame.

“Faida za Nishati Jadidifu ni pamoja na kupunguza gharama za kununua umeme mara kwa mara,kutoa ajira,kukaushia vyakula shambani,kuepuka matatizo ya kiafya kwa kuvuta hewa chafu,kupunguza hewa ukaa na kutunza tabaka la kuzuia mionzi ya jua

“Ili upate tani moja ya mkaa lazima ukate magogo 12 ya miti na kwa mwaka tunatumia tani Milioni 2.5 za mkaa nchini hivyo ni lazima tuendeleze kuhifadhi mazingira na kutumia nishati jadidifu kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo”amesema Sago

Hata hivyo Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET) chini ya Mkurugenzi wake John Chikomo kimeahidi kuendelea kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili kujikita zaidi katika kuandika habari za mazingira kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.

 

Next Post
Idadi ya watu yafikia bilioni nane,India kuipita China 2023

Idadi ya watu yafikia bilioni nane,India kuipita China 2023

TAWJA chaanza kutoa elimu kwa majaji,mahakimu

TAWJA chaanza kutoa elimu kwa majaji,mahakimu

Wanajeshi wa Kenya wawasili DRC kukabiliana na waasi

Wanajeshi wa Kenya wawasili DRC kukabiliana na waasi

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In