• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Sunday, January 18, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Kigahe:Wafanyabiashara tumieni teknolojia mbadala kukabili mabadiliko ya tabia nchi

by bajeti
December 6, 2022
in Mazingira
0
Kigahe:Wafanyabiashara tumieni teknolojia mbadala kukabili mabadiliko ya tabia nchi
Share on FacebookShare on Twitter

NA MIRIAM SARAKIKYA,ARUSHA

NAIBU Waziri wa Uwekezaji,Viwanda  na Biashara Exaud Kigahe amewataka Wafanyabiashara nchini wakiwemo wa makampuni ya Ndege na Sekta ya Utalii  kutumia teknolojia mbadala za kupunguza uchafuzi wa mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Kigahe ametoa kauli hiyo Desemba 5,2022 jijini Arusha wakati akizindua Maadhimisho ya Kitaifa ya Ushindani kwa mwaka 2022  jijini Arusha.

Amesema ni muhimu kwa wafanya biashara kutumia teknolojia za kisasa katika vyombo vya usafiri ili kuweza kutunza mazingira.

“Ilikupunguza ongezeko la mabadiliko ya tabia nchi naomba nitoe wito kwa makampuni kutumia teknolojia ili kutunza hewa safi ambayo ni rafiki pia kwa wanayama na binadamu “amesema Kigahe

Hata hivyo Kigahe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini amebainisha kuwa ukataji wa miti hovyo umekuwa ukichangia uharibifu wa mazingira na kuongeza kuwa ni muhimu kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa hifadhi za wanyamapori kupunguza ukataji wa miti kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii.

Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Mrisho Gambo amebainisha kuwa  kuna haja ya kutolewa kwa elimu zaidi kwa wafanya biashara wadogo ili waweze kukuza soko kwa kuingia kwenye ushindani mkubwa wa kibiashara kwa mataifa mengine.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (FCT) Jaji Salama Magimbi amefafanua kuwa Baraza hilo liliundwa kwa lengo la kudhibiti bidhaa bandia ili kukuza uchumi wa soko la Tanzania.

Katika Kilele cha maadhimisho hayo ambayo kitaifa yamefanyika jijini Arusha huku kaulimbiu ikiwa ni ‘Ushindani wa Utalii Endelevu’ lengo likiwa ni kuboresha Utalii hususani katika kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

 

Next Post
Serikali yaanza kutatua mgogoro wa vijiji na hifadhi ya Wembere

Serikali yaanza kutatua mgogoro wa vijiji na hifadhi ya Wembere

DODOMA

Zanzibar

Zanzibar

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:27
  • Today's page views 27
  • Total visitors 13,184
  • Total page views 14,930

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In