• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Wednesday, April 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Waliovamia Msitu wa Kuni watakiwa kuondoka

by bajeti
December 15, 2022
in Mazingira
0
Waliovamia Msitu wa Kuni watakiwa kuondoka

Baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja (hayupo pichani) wakati akizungumza nao kuhusu uvamizi katika Msitu wa Kuni uliopo katika eneo lao Desemba 15,2022 wakati wa ziara ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta(Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii )

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,MOROGORO

WANANCHI  waliovamia Hifadhi ya Msitu wa Kuni uliopo wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro na kuanzisha shughuli za ujenzi wa nyumba wametakiwa kusitisha na kuondoka mara moja katika eneo hilo ili kulinda ikolojia yake.

Kauli hiyo imetolewa  leo Desemba 15 na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wilayani humo..

“Sasa tunachowaomba kwanza msimamishe ujenzi kwenye eneo la msitu ,pili tutaangalia wale ambao wamejimilikisha maeneo makubwa ili tuyagawe  kwa sababu wote ni wavamizi” amesisitiza  Masanja.

Amesema Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa huruma yake aliruhusu eneo la msitu lenye jumla ya hekta 2000 limegwe ili kugawiwa kwa wananchi lakini wananchi wameendelea kulivamia eneo la msitu.

“Mwaka jana tulielekeza wananchi wapangwe kwenye hekta 2000 na hiyo ni huruma ya Mheshimiwa Rais Samia, naomba tumpongeze Mama yetu ana huruma  kwa sababu ilikuwa muondolewe lakini akasema hapana hawa ni wananchi wangu wapangwe” ameongeza Masanja.

Aidha amefafanua kuwa wananchi waliomo kwenye hekta 2000 zilizomegwa  wakagawiwa wako kihalali na watapimiwa ardhi na  kupewa hati zao lakini waliovamia wanapaswa kuondoka katika eneo hilo.Msitu wa Kuni unaomilikiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ulisajiliwa mwaka 1953 kwa tangazo la Gazeti la Serikali.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Fatma Mwassa, (wa kwanza kulia)Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki, Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mary Masanja wakiwa katika mkutano na wananchi katika Msitu wa Kuni uliopo Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ikiwa ni ziara ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta ya kutatua migogoro ya ardhi mkoani humo(Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)
Next Post
Wafanyabishara ya Kaboni watakiwa kusajili miradi yao

Wafanyabishara ya Kaboni watakiwa kusajili miradi yao

PWANI

PWANI

Masanja:TAWA fanyeni kazi kwa ushirikiano kufikia malengo

Masanja:TAWA fanyeni kazi kwa ushirikiano kufikia malengo

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:8
  • Today's page views 10
  • Total visitors 15,843
  • Total page views 17,958

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In