• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Mpango wa jamii kukabili athari za mabadiliko ya tabianchi waja nchini.

by bajeti
December 21, 2022
in Mazingira
0
Mpango wa jamii kukabili athari za mabadiliko ya tabianchi waja nchini.

Washiriki katika kikao kazi cha kutambulisha Mpango wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza Mitaji kwa ajili ya Maendeleo (UNCDF) kupitia mfumo wa kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi (LOCAL) kilichoandwaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais,wakimsikiliza Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Andrew Komba (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao hicho Desemba 21, 2022 ,jijini Dodoma.(picha na ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,DODOMA

OFISI ya Makamu wa Rais imetambulisha Programu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza Mitaji kwa ajili ya Maendeleo (UNCDF) kupitia mfumo wa kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi (LoCAL).

Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho Desemba 21, 2022 jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Mazingira Dkt. Andrew Komba amesema programu hiyo itaongezea jamii mtaji katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi ambayo yana athari kubwa katika maisha yao ya kila siku.

Dkt. Komba aliyemwakilisha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Switbert Mkama amesema programu hiyo awamu ya kwanza ya utekelezaji ipo katika Halmashauri tatu za Chamwino, Kondoa na Mpwapwa mkoani Dodoma ambapo baada ya kupata matokeo tarajiwa, itaendelea na kufikia hadi Halmashauri 10 mpaka 15 katika awamu wa pili ya programu.

Amesema Halmashauri hizo zilichaguliwa kutokana na mpango tayari uliokuwepo wa DCF kupitia UNCDF walifanya kazi katika maeneo hayo na kiasi cha fedha kilichotolewa kinalenga katika kupanua shughuli ambazo tayari zinaendeela kutekelezwa.

Ameongeza kuwa  kikao hicho ni fursa kwa washiriki kuweza kupitia taarifa mbalimbali za kimazingira zikiwemo biashara ya kaboni ambayo tayari Serikali imeandaa Mwongozo na Kanuni zake.

Kwa mujibu wa Dkt.Komba, kikao hicho kitawapa fursa ya kujadili kuhusu mchango wa kitaifa wa kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi (NDC), Tathmini ya athari ya Mazingira Kimkakati, Mpango Kabambe wa Taifa wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira na taarifa ya masuala Jangwa yanayoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

“Huu ni mwendelezo wa jitihada za kitaifa za kushughulikia athari za mabadiliko ya tabianchi na kulinda uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli za binadamu hususan katika serikali ya mitaa, vijiji na vitongoji” amefafanua Dkt Komba.

Aidha, Dkt. Komba amebainisha kuwa  nchi 24 duniani zinatekeleza programu hiyo huku Tanzania ikiwa mojawapo ambapo hukutanisha mawaziri wa kisekta wanaounda Bodi inayokutana kila mwaka kujadili namna ya kuwezesha jamii kukabili athari za mabadiliko ya tabianchi.

“Serikali inaamini programu hii italeta tija iwapo itakuwa na ufanisi kwasababu ni miongoni mwa programu zinazotambua dhana ya kuona fedha za mabadiliko ya tabianchi zinamfikia mlengwa moja kwa moja kwa maana kijiji husika” ameeleza  Dkt.Komba.

Kikao hicho cha siku mbili kinahusisha washiriki kutoka katika Wizara mbalimbali ambazo zinashughulikia Mpango huu wa LoCAL chini ya washirika wa maendeleo UNCDF.

 

Next Post
Senyamule:Anachokifanya Rais Samia ni kwa ajili ya watanzania wote

Senyamule:Anachokifanya Rais Samia ni kwa ajili ya watanzania wote

ARUMERU

ARUMERU

PWANI

PWANI

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:6
  • Today's page views 6
  • Total visitors 13,062
  • Total page views 14,807

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In