• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Bilioni 120 kutumika miradi ya uhifadhi wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi

by bajeti
February 14, 2023
in Mazingira
0
Bilioni 120  kutumika miradi ya uhifadhi wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi

Wadau na Wataalamu wa Mazingira wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa warsha ya kuainisha vipaumbele vya miradi ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi inayosimamiwa na Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) jijini Dodoma Februari 13, 2023.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,DODOMA

TANZANIA inatarajia kunufaika na mradi wenye thamani ya Sh.Bilioni 120 kwa ajili ya miradi ya uhifadhi wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi kutoka Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF).

Hayo yametangazwa Februari 13, 2023 jijini Dodoma na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mary Maganga wakati akifungua warsha ya Wadau na Wataalamu wa Mazingira inayolenga kuainisha vipaumbele vya miradi ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi inayosimamiwa na GEF.

Maganga amesema Tanzania ni nchi mnufaika kutoka GEF ambapo itapokea kiasi cha Sh.Bilioni 120 kwa ajili ya miradi ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi na kuwashukuru washirika hao wa maendeleo kwa kuandaa mpango huo wa utoaji wa fedha hizo ambazo hadi sasa tayari zimekwishatolewa kwa awamu na kusema kuwa zitasaidia katika juhudi za kuimarisha uhifadhi na usimamizi wa mazingira nchini.

Aidha Maganga amewataka wadau na wataalamu hao kutumia vyema ujuzi na uzoefu walionao katika kuimarisha mapambano na changamoto za mazingira zilizopo kwa lengo la kuhakikisha maandalizi na utekelezaji wa miradi chini ya GEF- awamu ya  nane inatekelezwa kwa wakati.

“Tanzania ni nchi mnufaika wa miradi ya GEF ambayo inafadhiliwa kupitia mikataba mbalimbali ya kimataifa, hivyo Ofisi ya Makamu wa Rais imeona umuhimu wa kuita wadau na wataalamu kutoka wizara na taasisi za kisekta kutoka mashirika mbalimbali ili kuweka mikakati ya pamoja na kufanikisha ajenda ya mazingira,” amesema Maganga.

Hata hivyo ametoa wito kwa wataalamu hao kuhakikisha wanafanya maandalizi ya haraka ya kuainisha maeneo ya kipaumbele ya miradi ya washirika wa maendeleo ili kuanza katika mwaka uliowekwa na kuikamilisha kwa wakati.

Kwa upande wake Mratibu wa GEF  Kanda ya Afrika  Ibrahima Sow amebainisha kuwa Tanzania imetengewa mgao huo wa fedha za mzunguko wa nane katika maeneo matatu ya mradi kwa kipindi cha miaka minne ijayo.

Sow ametaja maeneo hayo kuwa ni Mradi wa Usimamizi katika Maziwa Makuu na Mabonde ya Maji, fedha za kujenga uwezo kwa wataalamu wa miradi pamoja na usimamizi wa miradi katika nchi zinazoendelea.

Naye Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Andrew Komba amesema katika eneo la kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, Serikali imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali na kuhimiza na kuhamasisha utunzaji wa mazingira.

Ameongeza kuwa mabadiliko ya tabianchi ni miongoni mwa matokeo ya kuongezeka kwa gesijoto duniani sambamba na uharibifu wa uoto asili na bioanuai, hivyo Serikali imeanzisha kampeni za upandaji miti ili kuhakikisha nchi inakabiliana na athari hizo.

Next Post
Mtambo achangia ujenzi Zahanati ya Kijiji Dondo

Mhandisi Mtambo:Kuwe na uwazi katika utoaji tenda za ujenzi

Makamu wa Rais Dkt.Mpango awaonya maafisa watendaji,viongozi TARURA

Makamu wa Rais Dkt.Mpango awaonya maafisa watendaji,viongozi TARURA

GEF kuendelea kufadhili miradi ya mazingira

GEF kuendelea kufadhili miradi ya mazingira

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In