• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Makamu wa Rais Dkt.Mpango awaonya maafisa watendaji,viongozi TARURA

by bajeti
February 25, 2023
in Mazingira
0
Makamu wa Rais Dkt.Mpango awaonya maafisa watendaji,viongozi TARURA

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa Watendaji Kata kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wakati wa hafla ya kukabidhi Magari 54 kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na Pikipiki 916 kwa Watendaji Kata zilizotolewa na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),jijini Dodoma – Mtumba Februari 14, 2023.(Picha na Ofisi ya Makamu ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,DODOMA

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amewaasa Maafisa Watendaji Kata kuacha uzembe katika usimamizi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo na shughuli nyingine za kijamii.

Mbali na hilo lakini pia amewataka Watendaji wa Kata na Viongozi wa Mikoa wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) kutumia vitendea kazi wanavyokabidhiwa na serikali katika kuwafikia wananchi kwa urahisi, kuwasikiliza, kuwahudumia,kufuatilia miradi ya maendeleo  na siyo kutumia  kwa manufaa binafsi.

Makamu wa Rais amesema hayo Februari 14,2023 jijini Dodoma wakati wa hafla ya kukabidhi  magari 54  kwa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na Pikipiki 916 kwa Watendaji Kata zilizotolewa na Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),

Amesema utoaji wa vitendea kazi hivyo pamoja na mambo mengine  unalenga kuongeza ufanisi katika  ufuatiliaji wa  miradi ya maendeleo kwenye maeneo wanayosimamia.

Hata hivyo Dkt.Mpango amewaagiza maafisa watendaji kutambua na kushughulikia changamoto za wananchi kwa kuhakikisha vikao na wananchi katika ngazi ya Vijiji na Mitaa vinafanyika kama inavyopaswa.

“Ni muhimu kuzingatia uhifadhi wa mazingira kwa kutoa hamasa kwa wananchi ili wawe mstari wa mbele katika shughuli za uhifadhi ikiwemo kupanda miti na usafi wa mazingira ili kuwepo na  maendeleo endelevu.

“Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuimarisha mfumo na utendaji wa Serikali za Mitaa, kwa kuzingatia misingi ya Kikatiba na Kisheria iliyopo kwa kutambua kwamba, mfumo wa Serikali za Mitaa, ndio njia pekee ya kusogeza huduma karibu na wananchi lakini pia kuwashirikisha wananchi katika kuamua, kupanga na kuchagua vipaumbele vya maendeleo yao na ya Taifa kwa ujumla”amesema Dkt.Mpango

Dkt.Mpango amewataka pia Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha fedha kiasi cha Shilingi laki moja inayopaswa kutolewa kwa Maafisa Watendaji wa Kata kama posho ya madaraka inatolewa  kwa wakati na kupewa kipaumbele kabla  hazijalipwa posho za vikao vingine vya Halmashauri.

Akizungumzia TARURA,Dkt.Mpango amewataka ameutaka wakala huyo kufanya kazi kwa weledi na uaminifu ili kuyatimiza vema majukumu yao hususani ya kusimamia shughuli za ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara.

Amewasisitiza Mameneja wa Mikoa na Wilaya waliokabidhiwa magari hayo kutumia  katika  kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao na si vinginevyo pamoja na  kuyatunza na kuyafanyia ukaguzi na matengenezo ndani ya muda ili yaweze kudumu.

Kwa Upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Angellah Kairuki amesema Wizara hiyo itaendelea kuimarisha ngazi za msingi ikiwemo kata kwa kutambua ndiyo kiungo muhimu kati ya serikali na wananchi katika utoaji huduma.

Ameongeza kuwa mgao wa fedha zinazopatikana utaendelea kuelekezwa katika makundi hayo muhimu zaidi kuwawezesha katika kuratibu na kufuatilia shughuli za maendeleo katika maeneo ya vijiji, mitaa na vitongoji

Aidha Waziri Kairuki amebainisha kuwa lengo la vitendea kazi hivyo ni kuongeza ufanisi katika utoaji huduma kwa wananchi, kurahisisha usafiri pamoja na kuimarisha mapato.

“TAMISEMI inapanga kutumia biashara ya kaboni kama hatua ya kulinda mazingira pamoja na kuongeza vyanzo vya mapato kwa wananchi na Halmashauri kwa ujumla”amesema Kairuki

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Jenista Mhagama amesema Serikali inaendelea kulipa na kupandisha madaraja watumishi wa umma hapa nchini ambapo tayari kibali cha kupanda madaraja kwa watumishi 26491 ambao walisimama kwa muda mrefu kimetolewa.

Mhagama ameongeza kwamba serikali inatarajia kuongeza wahandisi pamoja na wakadiriaji majengo katika halmashauri ili kukabiliana na tatizo la ujenzi wa miundombinu chini ya kiwango.

“Serikali inathamini na itahakikisha kunakuwepo na  rasimimali watu ya uhakika ambayo ndiyo  chachu ya ujenzi wa uchumi”amesema Mhagama

Naye Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ametoa wito kwa serikali kufanya mapitio ili kutambua upande wenye tija katika ukusanyaji mapato hususani kodi ya majengo kati ya Serikali Kuu na TAMISEMI ili kupewa jukumu la ukusanyaji na kupata matokeo makubwa zaidi.

Chongolo amesema kumekuwepo na mabadiliko makubwa baada ya kuanzishwa kwa TARURA kwani Halmashauri zimeondokana na mgawanyo usio sawa wa mapato kulingana na mahitaji katika ujenzi wa miundombinu na sasa vipaumbele vinawekwa sehemu zenye changamoto zaidi.

 

 

Next Post
GEF kuendelea kufadhili miradi ya mazingira

GEF kuendelea kufadhili miradi ya mazingira

Putin:Kuishinda Urusi ni jambo lisilowezekana

Putin:Kuishinda Urusi ni jambo lisilowezekana

Vumbi laitesa Cameroon

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In