• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Vumbi laitesa Cameroon

by bajeti
February 21, 2023
in Mazingira
0
Share on FacebookShare on Twitter

YAOUNDE,CAMEROON

WAKATI Dunia ikiomboleza vifo vya watu zaidi ya 47,000 vilivyotokana na tetemeko la ardhi nchini Uturuki na Syria matatizo ya kimazingira yanaendelea kuikumba sayari ya Dunia katika maeneo tofauti ambapo nchini Cameroon vumbi  kutoka Jangwa la Sahara limeikumba nusu ya nchi hiyo.

Wakati hayo yakijiri vimbunga,ukame,mafuriko,ongezeko la joto pamoja na kuongezekana kwa maji ya bahari limekuwa jambo la kawaida kutangazwa na kusabisha vifo vya maelfu ya watu duniani lakini vumbi kusambaa nusu ya nchi limeonekana kuwa ni tofati na majanga mengine yanayoikumba dunia

Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida nchini Cameroon kumekuwa na vumbi la ajabu hali iliyosababisha serikali kutoa tahadhari juu ya janga hilo ambalo ni nadra kutokea duniani

Awali Februari 16,2023 Waziri wa Uchukuzi wa Cameroon Ernest Ngalle Bibehe amesema kiwango kikubwa cha vumbi kutoka Jangwa la Sahara kinatarajiwa kuathiri nusu ya Cameroon.

Bibehe, ameonya kuwa vumbi hilo linaweza kusababisha ajali za barabarani kutokana na kupunguza uwezo wa madereva kuona mbali na  kusababisha matatizo ya kupumua.

Hata hivyo vumbi kubwa linaendelea kushuhudiwa nchini humo kwa sasa katika eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo na huenda likaathiri maeneo mengine na kutolewa tahadhari ikiwataka watu kuendesha magari kwa umakini na kufunika macho pamoja na pua.

Cameroon inadaiwa kushuhudia kiwango kikubwa cha vumbi kutoka Jangwa la Sahara kila mwaka, hasa sehemu za Kaskazini na Kusini.

 

Next Post
CCM yawaonya wafanyabishara,wawekezaji wanaokwepa kodi

CCM yawaonya wafanyabishara,wawekezaji wanaokwepa kodi

Boeing yasitisha  ndege za Dreamliner -787

Boeing yasitisha ndege za Dreamliner -787

Mazungumzo

Mazungumzo

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:5
  • Today's page views 5
  • Total visitors 13,061
  • Total page views 14,806

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In