• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Mhandisi Mtambo:Kuwe na uwazi katika utoaji tenda za ujenzi

by bajeti
February 14, 2023
in Habari
0
Mtambo achangia ujenzi Zahanati ya Kijiji Dondo

Waziri Kivuli wa Miundombinu wa Chama cha ACT-Wazalendo Mhanidi Mohamed Mtambo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kushiriki katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,PWANI

WAZIRI Kivuli wa Miundombinu kutoka Chama cha ACT-Wazalendo Mhandisi Mohamedi Mtambo amesema ni muhimu kuwepo na uwazi katika utoaji wa kandarasi za ujenzi ikiwemo barabara ili wananchi waweze  kujua fedha zilizotolewa na Rais zinatumika katika viwango vinavyohitajika.

Mhandisi Mtambo ametoa kauli hiyo Februari 14,2023 Mkuranga mkoani Pwani wakati akizungumza kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini ikiwemo ya Soko,Barabara  Vituo vya Afya na Zahanati.

 

Amesema kumekuwa na usiri kati ya mtoa kandarasi na mkandarasi hivyo kupelekea miradi hiyo kushindwa kusimamiwa vema na wananchi na kujengwa chini ya kiwango.

“Mimi kama Waziri Kivuli wa Miundominu ikiwemo Ujenzi, Barabara na Reli, kutoka Chama changu cha ACT-Wazalendo tunataka kuwepo na uwazi kati ya mtoa kandarasi na mkandarasi ili kujua kiwango cha fedha zitakazotumika katika ujenzi huo,aina ya barabara inayojengwa na viwango vyake kama ni lami basi ijulikane ni ya kiwango gani,lakini pia tenda itolewe eneo husika.

“Ufunguzi pia ufanyike eneo husika kwa kuwahusisha Viongozi wa Serikali za Mitaa,Diwani na wananchi jinsi mradi huo utakavyotekelezwa katika eneo lao au utapita katika eneo lao hali itakayosaidia wananchi kulinda na kufuatilia kwa ukaribu lakini sio tenda inatolewa eneo lingine na ujenzi unafanyika eneo lingine.

“Tungependa kuona mabango yote ya wakandarasi yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili ili wananchi waelewe na kufuatilia kwa karibu”amesema Mhandisi Mtambo

Mtambo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama hicho Mkoa wa Pwani ameongeza kuwa wao wanaamini kuwa Taifa la wote na maslahi kwa wote  hivyo uwazi utasaidia uwajibikaji na sio wananchi kuona mkandarasi akifikisha vifaa vya ujenzi eneo la mradi bila kujua kitakachojengwa, gharama zake na viwango vitakavyotumika katika ujenzi.

“Mfano kama unajenga barabara ya Mbande hadi Mbagala sasa hapa kandarasi itangazwe kwa uwazi na waanchi na viongozi wa Mbagala pamoja na Chamanzi  na Mbane wajue,lakini pia wajue gharama zake,viwango vya ujenzi huo na uzinduzi ufanyike maeneo yao ikiwemo bango la ujenzi kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili na sio lugha ya kiingereza”ameongeza Mtambo

Mtambo amebainisha kuwa kwa kufanya hivyo kutawafanya wananchi kushiriki na kulinda miradi hiyo ikiwemo kukosoa pale wanapoona hapaendi sawa kulingana na uwazi waliopata hivyo kusaidia fedha zinazotolewa kwa ajili ya ujenzi kutumika inavyokusudiwa.

 

Next Post
Makamu wa Rais Dkt.Mpango awaonya maafisa watendaji,viongozi TARURA

Makamu wa Rais Dkt.Mpango awaonya maafisa watendaji,viongozi TARURA

GEF kuendelea kufadhili miradi ya mazingira

GEF kuendelea kufadhili miradi ya mazingira

Putin:Kuishinda Urusi ni jambo lisilowezekana

Putin:Kuishinda Urusi ni jambo lisilowezekana

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:5
  • Today's page views 5
  • Total visitors 13,061
  • Total page views 14,806

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In