• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Sayansi,Utafiti na Ubunifu vyasisitizwa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050

by bajeti
April 7, 2023
in Habari
0
Sayansi,Utafiti na Ubunifu vyasisitizwa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050

Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango akiwapungia mkono viongozi mbalimbali wa Serikali hawapo (pichani) jijini Dodoma Aprili 4,2023 wakati wa uzinduzi wa Dira ya Maendeleo 2050.Kulia ni Waziri wa Fedha Dkt.Mwigulu Nchemba na wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Daniel Chongolo

Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

RAIS Samia Suluhu Hassan amependekeza vipaumbele sita muhimu kuwepo katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ikiwemo Elimu hususani Sayansi,Utafiti na Ubunifu ili kukuza ujuzi na uwezo wa nguvukazi ya Taifa.

Mbali na hilo lakini pia amesisitiza kuimarisha uwezo wa uchumi uliojengwa hadi sasa na mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Dira ya 2025, pamoja na  kutumia fursa ambazo hazijatumiwa ipasavyo hadi sasa na kuzikamata fursa zinazochipukia.

Kauli hiyo ya Serikali inaenda sambamba na kazi za Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) katika kuinua na kuibua bunifu za kisayansi na kitekonolojia zinazobuniwa na watanzania ili kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii.

Hata hivyo COSTECH chini ya Mkurugenzi wake Dkt.Amos Nungu Hata hivyo Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) chini ya Mkurugenzi wake Dkt.Amos Nungu imekuwa na jukumu la kukusanya,kuchakata,kuhifadhi na kusambaza,taarifa na kuishauri Serikali kuhusu masuala ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu ikiwemo vipaumbele vya utafiti.

Machi 7,2023 COSTECH iliandaa Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kati ya waandishi wa habari na watafiti ili kuisadia jamii kufahamu teknolojia na tafiti mbalimbali ambazo serikali imekuwa ikiwekeza kwa ajili ya kutatua changamoto za watanzania na kujitegemea na teknolojia yake kwa miaka ijayo.

Akizungumza jijini Dodoma Aprili 4,2023 wakati wa ufunguzi wa hafla ya Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango amesema Tanzania imefikia kipindi muhimu cha mageuzi ya kiuchumi na kijamii.

Amesema kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi ya wastani wa asilimia 6.6 kwa mwaka kwa kipindi cha miaka 20 mfululizo (2000-2019) kabla ya janga la ugonjwa wa UVIKO – 19, ilipelekea Benki ya Dunia (WB)kuitangaza Tanzania kuingia kwenye kundi la nchi za pato la kati ngazi ya chini Dola za Marekani 1,036 hadi 4,045 mwaka 2020

Amesema malengo makuu ya Dira 2025 yalikuwa matano ikiwemo Maisha Bora kwa kila Mtanzania,Kudumisha Amani,Usalama na Umoja katika Nchi,tatu ilikuwa ni Utawala Bora  na nne ni Jamii iliyoelimika vyema na inayojifunza,na tano ni uchumi imara na shindani.

“Lakini pamoja na hatua kubwa iliyofikiwa, nchi yetu bado imeendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali zilizopelekea malengo ya Dira ya 2025 kutofikiwa kwa ukamilifu;mfano tumeendelea kukabiliwa na changamoto ya umaskini wa kipato na lishe duni ambapo  takriban asilimia 26.4 ya Watanzania wote bado wanaishi chini ya kiwango cha umaskini wa kipato na wananchi maskini zaidi wanaishi vijijini wakiwa ni asilimia 31.3”amesema Dkt.Mpango

Dkt.Mpango amebainisha kuwa Dira mpya itakayoanza kuandaliwa baada ya uzinduzi huo inategemewa kuakisi maono, matamanio na mitazamo ya Watanzania kuhusu mustakabali wa nchi yao katika kipindi cha miaka 25 ijayo.

“Naishukuru Wizara ya Fedha na Mipango kwa kumualika Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa Mgeni Rasmi katika hafla hii muhimu sana ya Kuzindua Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

“Hata hivyo, kutokana na majukumu mengine ya kitaifa aliyonayo, amenipa heshima nimuwakilishe  na Mheshimiwa Rais anawapongeza sana Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na wadau mbalimbali, kwa kuanza mchakato huu wa kuandika maono na matamanio ya watanzania kuhusu matumizi bora kabisa ya rasilimali na fursa za nchi ili kuiwezesha Tanzania kustawi kuwa miongoni mwa nchi zenye kipato cha juu ifikapo 2050”amesema Dkt.Mpango

Ameongeza kuwa ni ni Dira inayotarajiwa kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii ili kufikia lengo la kuwa Taifa lenye ustawi,hivyo, ni dhamira ya Serikali kuwa katika maandalizi ya Dira hiyo ambapo Watanzania kutoka pembe zote za nchi na matabaka mbalimbali ya maisha watapata nafasi ya kuchangia mawazo yao

Aidha amefafanua kuwa kwa kuzingatia baadhi ya changamoto alizozitaja na mabadiliko ya haraka yanayoendelea duniani, hususani ya kiteknolojia, kiuchumi, na mazingira ni vyema maandalizi ya Dira 2050 pamoja na mambo mengine yazingatie yafuatayo:

“Jambo la kwanza:Ni kuimarisha uwezo wa uchumi uliojengwa hadi sasa na mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Dira ya 2025;Jambo la Pili:Kutumia fursa ambazo hatujazitumia ipasavyo hadi sasa na kuzikamata fursa zinazochipukia;Kwa mfano katika Kilimo, Tanzania ina fursa kubwa ya kuwa ghala la chakula katika Bara la Afrika au hata Mashariki ya Kati, tukilenga uzalishaji mkubwa wa mahindi, ngano, shayiri, soya, sukari, mafuta ya kupikia, korosho, matunda, mbogamboga, na viungo (spices) n.k.;

“Mifugo na uvuvi: uwekezaji katika viwanda vya nyama, maziwa, ngozi, uzalishaji wa malisho na chakula cha mifugo na pia uvuvi na ufugaji wa samaki na uchakataji wake,Mazao ya Misitu: viwanda vya bidhaa za mbao, nyuki na dawa

“Jambo la Tatu muhimu sana;Elimu hususan sayansi, ufundi na ufundi stadi, utafiti na maendeleo, na ubunifu ili kukuza ujuzi na uwezo wa nguvukazi ya Taifa”amesema Dkt.Mpango

Dkt.Mpango ametaja Jambo la Nne kuwa  ni namna ya kuvutia na kuasili teknolojia ili kukuza tija katika sekta zote za uzalishaji na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ikiwa pamoja na kuingia ubia wa kimkakati kuiwezesha Tanzania kuwapita washindani wake katika kipindi kifupi (leapfrog).

“Jambo la Tano ni kubaini kiuhalisia rasilimali zote zinazohitajika kuwezesha utekelezaji makini (usio wa mazoea) wa Dira na mipango na kubainisha mfumo thabiti wa ufuatiliaji na tathmini kwa kuangalia vigezo mahususi vilivyowekwa (key performance indicators).

”Jambo la Sita ni kujifunza kutoka katika nchi zilizofanikiwa kuendelea kwa kasi kuanzia miaka ya 1960, hususan zile za Asia”amebainisha Dkt.Mpango

Kwa upande wa kudumisha amani, usalama na umoja, Dkt.Mpango ameeleza kuwa Tanzania inajivunia kuwa Kisiwa cha Amani.

“Nchi yetu imeendelea kuwa na amani, utulivu, umoja, mshikamano na ni ya mfano katika Bara la Afrika,hata hivyo, ni lazima tuendelee kuzilinda na kuzitunza tunu hizi katika kipindi cha miaka 25 ya Dira mpya kwa sababu bila Amani, usalama na umoja hakuna maenedeleo”ameongeza Dkt.Mpango

COSTECH kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2018 hadi 2022 imefanikiwa kuwatambua wabunifu katika masuala ya sayansi na teknolojia zaidi ya  2647 ambapo  kiasi cha Sh.Bilioni 4.26 zimetumika kwa wabunifu 178 kuwezeshwa  ili waweze kuendeleza vitu walivyobuni kwa manufaa ya kuwanufaisha wananchi.

Next Post
DODOMA

Bashe:Hatutumii GMO lakini hatuwezi kuacha kuijua

Wafugaji wapewa madume bora 366 ya ng’ombe kuboresha mifugo yao

Wafugaji wapewa madume bora 366 ya ng’ombe kuboresha mifugo yao

COSTECH yatoa Sh.Milioni 250 kwa mbunifu wa mita za maji kuanzisha kiwanda.

COSTECH yatoa Sh.Milioni 250 kwa mbunifu wa mita za maji kuanzisha kiwanda.

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In