• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Mwanafunzi kidato cha kwanza atengeneza redio

by bajeti
April 12, 2023
in Habari
0
Mwanafunzi kidato cha kwanza atengeneza redio

Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari Chumbageni iliyopo jijini Tanga Adinan Sadik akitengeneza redio inayoshika vituo mbalimbali vya redio.(Picha na mpigapicha wetu)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,TANGA

MWANAFUNZI wa Kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Chumbageni jijini Tanga Adinan Sadik ametengeneza redio na vifanya vingine vya kieletroniki ikiwemo helkopta ambayo inadaiwa kuwa iliruka baada ya kuwekwa mota.

Mwanafunzi huyo ambaye anaonekana kuwa Mtafiti na Mbunifu amebuni pia kifaa cha kieletroniki ambacho kitatumika kuchomea dawa za mbu na udi ambapo ubunifu huo umethibitishwa pia na Diwani wa Kata ya Chumbageni Ernest Kimaya.

Akizungumza na tovuti hii ya Bajeti,Sadick amesema yeye anaweza kutengeneza vitu vinavyotumika na binadamu lakini anahitaji kusaidiwa zaidi ili kufikia ndoto zake za kuwa mwanasayansi.

“Nimetengeneza redio mbili na zinashika vituo vyote na sijafundishwa na mtu hivyo naomba nisaidiwe ili niweze kufikia malengo yangu”amesema Sadik

Kwa upande wake Mwalimu wa Somo la Sayansi katika Shule hiyo Burhan Kumba amesema mwanafunzi huyo ana kipaji kikubwa cha kutengeneza vitu vya kieletroniki na kwamba ametengeneza redio inayoshika vituo mbalimbali kwa kutumia boxi na waya za kawaida.

“Sisi kama walimu tulifanya jitihada za kuhakikisha wadau wa Elimu Mkoa wa Tanga wanafahamu taarifa za kuwepo kwa mwanafunzi huyu na vitu anavyobuni na kuvitengeneza lakini hadi sasa bado hatujapa muendelezo wake tangu tulipofikisha taarifa hizi”amesema Kumba

Kumba amesema wao kama walimu wameona ana kipaji cha hali ya juu hivyo walipendekeza pia kupelekwa katika shule za ufundi  ili aweze kuendeleza ubunifu na kipaji chake ambapo pia waliwashirikisha wazazi wake katika kumsaidia.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Chumbageni Ernest Kibaya amesema jitihada zinaendelea za kumsaidia mwanafunzi huyo ili aweze kufikia lengo lake na kusaidia wengine kutokana na kipaji chake.

Hata hivyo Tume ya Raifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imekuwa ikishindanisha wabuni wa kisayansi  na kiteknolojia katika mashindano maarufu kama MAKISATU ambapo washindi mbalimbali hujipatia zawadi na kuendelezwa kwa bunifu zao.

Next Post
MUUNGANO

DODOMA

Jeshi la Polisi latakiwa kujitathmini kukabiliana na mabadiliko ya kiteknolojia.

Jeshi la Polisi latakiwa kujitathmini kukabiliana na mabadiliko ya kiteknolojia.

Matembezi

Matembezi

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:6
  • Today's page views 6
  • Total visitors 13,062
  • Total page views 14,807

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In