• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Siasa

CCM yaunga mkono Rais Dk.Mwinyi kuongeza pensheni kwa wastaafu

by bajeti
May 18, 2023
in Siasa
0
CCM yaunga mkono Rais Dk.Mwinyi kuongeza pensheni kwa wastaafu

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar,kimepongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi,kwa maamuzi yake ya kupandisha viwango vya pencheni za wastaafu pamoja na za jamii kwa wazee wenye umri wa miaka 70.

Pongezi hizo zimetolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis mara tu baada ya Rais Dk.Mwinyi, kutangaza viwango hivyo katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi kitaifa yaliyofanyika Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Mbeto, amesema hatua hiyo ni ya kupongezwa na imeandika historia kubwa katika falsafa ya utawala bora kwani mara nyingi wananchi wanaostaafu wamekwa hawapewi kipaumbele.

Amesema matunda hayo yanatoka na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025 ambayo imetekelezwa kwa ufanisi mkubwa na kukuza uchumi ulitoa fursa ya kupatikana kwa fedha za kuimarisha miradi mbalimbali ya kijamii ikiwemo kuongeza pencheni hizo.

Ameongeza kuwa Dk.Mwinyi,ameendelea kuwa kiongozi mwenye maono,utu,huruma na mzalendo wa kweli katika kusimamia haki na kuimarisha maisha ya wananchi wa makundi mbalimbali nchini.

“Tunampongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Mwinyi, kwa maamuzi yake ya kuongeza kiwango cha pensheni kwa wastaafu waliotumikia nchi kwa uadilifu mkubwa.

“Hatua hii ni miongoni mwa mikakati,sera na vipaumbele vya CCM katika kuinua hali ya maisha ya wananchi wa makundi mbalimbali nchini.

“Maamuzi hayo ya kuongeza pensheni kwa wastaafu wa kima cha chini kwa asilimia 100 ambapo mstaafu aliyekuwa akipokea kiasi cha Sh. 90,000/= atapokea Sh. 180,000/= na kwa upande wa pensheni jamii imepanda kwa asilimia 150 kutoka Sh. 20,000/= hadi Sh. 50,000/= kwa Wazee wenye umri wa miaka 70 ambapo mabadiliko hayo ya pensheni yataanza katika mwaka wa fedha wa 2023/2024 ” amesema Mbeto

Aidha ameeleza kuwa Dk.Mwinyi, mbali na kuongeza kiwango hicho cha pencheni pia ameahidi kuyafanyia kazi mapendekezo mbalimbali yaliyotolewa na Chama cha wafanyakazi Zanzibar.

Naye Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM Zanzibar Khadija Salum Ali, ameongeza kuwa hatua hiyo ya Rais Dk.Mwinyi ya kuongeza pensheni inatakiwa kuenziwa kwa vitendo kwani imejenga faraja na hamasa kubwa kwa wastaafu mbalimbali nchini.

Next Post
Wananchi waendelea kunufaika na Mradi wa EBARR

Wananchi waendelea kunufaika na Mradi wa EBARR

Dkt.Mpango:Mawakili wachukuliwe hatua kali za kisheria

Dkt.Mpango:Mawakili wachukuliwe hatua kali za kisheria

Kero zilizobaki za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kushughulikiwa

Kero zilizobaki za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kushughulikiwa

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:8
  • Today's page views 8
  • Total visitors 13,064
  • Total page views 14,809

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In