• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Dkt.Mpango:Mawakili wachukuliwe hatua kali za kisheria

by bajeti
May 11, 2023
in Habari
0
Dkt.Mpango:Mawakili wachukuliwe hatua kali za kisheria

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiagana na Rais anayemaliza muda wake wa Chama Cha Mawakili Tanganyika (TLS) Prof. Edward Hoseah Mei 11,2023 jijini Arusha mara baada ya kuhitimisha hafla ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS)(Picha na Ofisi ya Makamu ya Makamu wa Rais).

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,ARUSHA

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa Chama Cha Mawakili Tanganyika (TLS) na Kamati ya Mawakili kuchukua hatua kali za kinidhamu na kisheria dhidi ya mawakili wachache wanaoharibu taaluma ya sheria kwa kukosa uadilifu na maadili mema.

Dkt.Mpango amesema hayo Mei 11,2023 wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) unaofanyika jijini Arusha.

Amesema kumekuwa na tuhuma kwa baadhi ya Mawakili kujihusisha na vitendo vya rushwa na udanganyifu kwa maslahi yao binafsi ikiwemo kuwasaliti wateja kwa kupokea rushwa kutoka upande wa pili na kuharibu kesi.

Hata hivyo Dkt.Mpango ameitaka TLS kuhakikisha inashirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria kutoa elimu kwa umma kuhusu suala la mihuri ya kielektroniki ili kuondokana na suala la vishoka na mawakili wanaotumia mihuri isiyo halali kufanya kazi za uwakili ikiwemo taasisi zote za serikali na binafsi kuhakikisha zinatumia mihuri ya kielektroniki ili kuondokana na kadhia hiyo.

Dkt.Mpango amefafanua kuwa ni wajibu wa sekta na taasisi za sheria kuendelea kuchambua, kubaini na kutoa mapendekezo ya sheria zinazotakiwa kufanyiwa marekebisho au kuandikwa upya hapa nchini.

Ameongeza  ni vema kuweka  nguvu zaidi katika kutoa elimu ya sheria kupitia mihadhara, redio, televisheni na mitandao ya kijamii ili kuondoa adha ya watu wengi wanaopoteza haki zao kwa kukosa uelewa wa sheria.

“Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha wananchi wake wanatendewa haki kwa mujibu wa sheria na kuishi kwa amani na utulivu katika nchi yao”amesema Dkt.Mpango

Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amewataka wanachama wa TLS kushiriki kikamilifu katika mchakato wa katiba mpya pamoja na mchakato wa mabadiliko ya sheria zinazohusiana na siasa, uchaguzi na demokrasia.

Amesema wanachama hao ni wadau muhimu katika kuhakikisha inapatikana Katiba Mpya itakayoweza kusaidia taifa miaka mingi ijayo hivyo  amewakaribisha katika kutoa ushauri pamoja na ushirikiano kwa kuwa serikali ipo tayari katika kutumia uzoefu na ujuzi wa wanachama wa chama hicho.

Akizungumza juu ya  utendaji wa TLS, Rais anayemaliza muda wake wa chama hicho Prof. Edward Hoseah amesema uongozi wa TLS umeweka muhimu na kipaumbele katika kuwa na ushirikiano wenye kujenga na serikali pamoja na wadau ambao umekuwa na manufaa makubwa kwa pande zote mbili.

Aidha amebainisha kuwa ushirikiano huo umefanya chama hicho kushiriki katika maboresho mbalimbali ya sheria hapa nchini ikiwemo kushiriki katika tume mbalimbali zinazoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo kikosi kazi cha kutathimini hali ya siasa na demokrasi nchini pamoja na tume ya maboresho ya mfumo wa taasisi za haki jinai.

Prof. Hoseah ameishukuru serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwezesha Chama hicho kupata ada za leseni na mahafali ambazo zilikua hazifiki katika chama hicho kinyume na sheria.

“Ushirikiano wa kujenga kati ya TLS na Serikali umewezesha kupatikana kwa kiwanja katika eneo la Mtumba mkoani Dodoma pamoja na kupungua kwa wimbi la kukamatwa kwa mawakili hapa nchini”amesema Prof.Hoseah

 

Next Post
Kero zilizobaki za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kushughulikiwa

Kero zilizobaki za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kushughulikiwa

Wachina kulipa nauli kupitia kiganja cha mkono

Wachina kulipa nauli kupitia kiganja cha mkono

MISRI

MISRI

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In