BEIJING,CHINA
NDEGE kubwa ya abiria ya aina ya C919, iliyotengenezwa na China kwa kujitegemea, ilikamilisha safari yake ya kwanza ya kibiashara kutoka Shanghai hadi Beijing, na kuashiria kuingia rasmi katika soko la usafiri wa anga.
Kwa mujibu wa taarifa ya Tovuti ya CRI ya nchi hiyo,imeeleza kuwa Ndege hiyo ya Shirika la Ndege la China Eastern iliruka asubuhi ya Mei 28,2023 kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Shanghai Hongqiao ikiwa na abiria 128, na kufika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing mchana.
Mkurugenzi wa Idara ya Masoko na Mauzo ya Shirika la Ndege la Kibiashara la China (COMAC) Zhang Xiaoguang amesema safari hiyo ya kwanza ni sawa na sherehe ya kuja kwa ndege mpya.
Amesema ndege hiyo itaendelea kuwa bora kama ikihimili changamoto za soko.
Hii ni ndege ya kwanza ya China iliyotengenezwa kwa mujibu wa vigezo vya kimataifa huku nchi hiyo ikiwa na haki zote za uvumbuzi.
Mafanikio ya nchi hiyo katika masuala ya anga yanaweza kuleta changamoto kwa makampuni mengine ya ndege ambayo hufanya biashara dunia nzima hivyo mafanikio ya nchi hiyo yanaweza kusaidia upatikanaji wa ndege za abiria kwa gharama nafuu.




Discussion about this post