• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

“Lima chakula sio tumbaku.” huua watu milioni nane kwa mwaka

by bajeti
May 31, 2023
in Mazingira
0
“Lima chakula sio tumbaku.” huua watu milioni nane kwa mwaka
Share on FacebookShare on Twitter

GENEVA,USWISI

KILA ifikapo Mei 31 ya kila mwaka Dunia huadhimisha siku ya kupinga matumizi ya tumbaku ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa  la Afya duniani (WHO), limezitaka nchi kuacha kutoa ruzuku kwa kilimo cha tumbaku na badala yake kuunga mkono na kusaidia kilimo cha mazao endelevu yatakayoweza kulisha mamilioni ya watu wenye uhitaji wa chakula.

Katika ujumbe wake wa siku hii ya kupinga matumizi ya tumbaku alioutoa Mei 31,2023, na kutangazwa na tovuti ya Umoja wa Mataifa ya UN Kiswahili,Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus amesema tumbaku inawajibika kwa vifo milioni nane kila mwaka  lakini bado serikali duniani kote zitatumia mamilioni ya dola kuunga mkono mashamba ya tumbaku.

Amesema watu duniani kote wanakabiliwa na njaa wakati ekari milioni 300 za dunia zinatumika kulima tumbaku.Ghebreyesus

 “Ni wakati wa kubadili mwelekeo wa juhudi zetu na kujikita na kilimo ambacho kinastawisha siha yetu na mazingira yetu.”amesema Ghebreyesus

Amesema WHO inafanyakazi kwa karibu na mashirika mengi ya Umoja wa Mataifa likiwemo la Chakula na Kilimo (FAO) na la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kuwasaidia wakulima kuhamia kwenye kilimo mbadala wa tumbaku

“kwa kuchagua kulima chakula badala ya tumbaku tutatoa kipaumbele kwa afya, kulinda mfumo wa maisha na kuimarisha uhakika wa chakula kwa wote.”amesema Ghebreyesus

Lengo la maadhimisho ya mwaka huu ni kuujulisha umma hatari za matumizi ya tumbaku, mwenendo wa biashara wa makampuni ya tumbaku, nini kinachofanywa na WHO kupambana na janga la tumbaku na nini watu duniani kote wanaweza kufanya ili kudai haki yao ya afya,  maisha yenye afya na kuvilinda vizazi vijavyo.

Siku ya kupinga matumizi ya tumbaku duniani huadhimishwa kila mwaka Mei 31 na mwaka huu imebeka maudhui “Lima chakula sio Tumbaku”

 

Next Post
Tanzania kupanda miti milioni 276 kila mwaka

Tanzania kupanda miti milioni 276 kila mwaka

Urusi yaizamisha meli ya kivita ya Ukraine kwa makombora

Urusi yaizamisha meli ya kivita ya Ukraine kwa makombora

Serikali yawaonya wafanyabishara bidhaa za plastiki

Serikali yawaonya wafanyabishara bidhaa za plastiki

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:9
  • Today's page views 9
  • Total visitors 13,065
  • Total page views 14,810

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In