• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Serikali yawaonya wafanyabishara bidhaa za plastiki

by bajeti
June 2, 2023
in Mazingira
0
Serikali yawaonya wafanyabishara bidhaa za plastiki

Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde (katikati) akifanya usafi wa mazingira katika eneo la Makole, Manispaa ya Dodoma Juni 2, 2023 ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani inayotarajia kuadhimishwa duniani kote ifikapo Juni 5 mwaka huu.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,DODOMA

SERIKALI imewaonya wafanyabiashara wachache wanaoendelea kuingiza, kuzalisha na kusambaza bidhaa za plastiki  zisizokidhi viwango ambzo zinazotumika kama vifungashio na kusababisha uchafuzi wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza Juni 2, 2023 jijini Dodoma katika zoezi la usafi wa mazingira katika kuelekea kilele cha Siku ya Mazingira Duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Juni 5 ya kila mwaka,Naibu Waziri wa Kilimo, Antony Mavunde amesema ni wajibu wa Wafanyabiashara kushirikiana na taasisi za Serikali katika kusimamia usitishaji wa Matumizi ya bidhaa za plastiki.

“Kumekuwa na juhudi mbalimbali za Serikali na wadau katika kukabiliana na uchafuzi wa mazingira utokanao na taka za plastiki, hata hivyo bado kuna ukiukwaji wa sheria kwa baadhi ya wafanyabiashara wanaoingiza na kuzalisha mifuko ya plastiki isiyokidhi viwango ambayo inayotumika madukani na watoa huduma” amesema Mavunde.

Hata hivyo Mavunde amewaka wananchi kuendelea kuiunga mkono Serikali katika kudhibiti matumizi ya mifuko na bidhaa za plastiki kwa kutoa ushirikiano kwa viongozi wa serikali za mitaaa ili kurahisisha zoezi hilo la kutokomeza vifungashio visivyokidhi viwango ambavyo vimekuwa visambazwa kupitia njia za panya.

Aidha Mavunde amesema Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imeendelea kufanya jitihada kubwa za kuhamasisha suala la utunzaji na uhifadhi wa mazingira katika maeneo ya miji mikuu nchini ikiwemo Jiji la Dodoma, hivyo ni wajibu wa wananchi wote nchinin kutosubiri Kilele cha Maadhimisho ya mazingira katika kujishughulisha na suala la usafi katika maeneo yao.

Awali akimkaribisha Mgeni rasmi, Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Switbert Mkama amesema katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani, Ofisi hiyo imejipanga kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma hatua inayolenga kupendezesha taswira ya Jiji hilo ambalo ni makao makuu ya Serikali.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Godwin Gondwe amesema Mkoa huo utaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuhakikisha kuwa Jiji la Dodoma ambalo ni Makao Makuu ya Serikali linaendelea kuwa safi.

Kilele cha Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo ina kauli mbiu isemayo “Pinga Uchafuzi wa Mazingira unaotokana na Taka za Plastiki”

 

Next Post
SMZ yawarudisha shule watoto 28,981 walioacha  masomo

SMZ yawarudisha shule watoto 28,981 walioacha masomo

Kaliua kufanya  biashara ya Kaboni baada ya kuanzisha misitu ya hifadhi

Kaliua kufanya biashara ya Kaboni baada ya kuanzisha misitu ya hifadhi

Utafiti:Watoto walionyonya maziwa ya mama hufaulu zaidi shuleni

Utafiti:Watoto walionyonya maziwa ya mama hufaulu zaidi shuleni

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In