• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Utafiti:Watoto walionyonya maziwa ya mama hufaulu zaidi shuleni

by bajeti
June 10, 2023
in Habari
0
Utafiti:Watoto walionyonya maziwa ya mama hufaulu zaidi shuleni

Mtoto akinyonya maziwa ya mama yake

Share on FacebookShare on Twitter

LONDON,UINGEREZA

WATAFITI  kutoka  Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza wametoa matokeo ya utafiti walioufanya na kuonesha kuwa wanafunzi waliotumia maziwa ya mama zao wakiwa wachanga hupata alama bora zaidi katika shule za upili.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa Juni 8,2023 na kituo cha habari cha parstoday.ir imeeleza kuwa kulingana na matokeo ya utafiti wa chuo hicho yameonesha kuwa wanafunzi ambao walinyonyeshwa kwa angalau miezi minne, wanapata kwa wastani, alama mbili hadi tatu zaidi kuliko wanafunzi ambao hawakunyonyeshwa na mama zao.

Mbali na hilo lakini pia, wanafunzi walionyonyeshwa kwa maziwa ya mama huwa wanafaulu masomo mengi zaidi na hivyo kufaulu zaidi kuingia vyuo vikuu.

Watafiti wa Chuo Kikuu cha Oxford wanasema kwamba walichunguza alama za kitaaluma za takribani wanafunzi 5,000 waliozaliwa kati ya 2000 na 2002 kwa muda mrefu ili kuchunguza uhusiano kati ya kunyonya mazima ya mama na alama zao za shule ya sekondari

Utafiti huo umeonesha kuwa, hata wakati masuala kama vile uwezo wa kiakili na hali ya kijamii na kiuchumi ya wanafunzi vilipozingatiwa, wanafunzi walionyonya mazima ya mama zao walikuwa na hali bora zaidi ya kimasomo na kitaaluma na walipata alama za juu katika shule za sekondari.

Mtaalamu kutoka taasisi ya  Nuffield Department of Population Health   Reneé Pereyra-Elías amesema kuwa mafanikio bora ya kielimu ni “moja tu” ya matokeo mazuri ya watoto wanaonyonya mazima ya mama zao, na kwamba maziwa ya mama yanapaswa kutolewa kwa mtoto kwa sababu husaidia “ustawi wa utambuzi” wa mtoto kwa kusaidia ukuaji wake wa neva.

Matokeo ya utafiti huu pia yamechapishwa katika jarida la “Archives of Disease in Childhood”.

 

Next Post
Wabunge watakiwa kuwa mstari wa mbele katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira

Wabunge watakiwa kuwa mstari wa mbele katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira

CCM Zanzibar ‘yamlilia’ Mohamed Raza

CCM Zanzibar ‘yamlilia’ Mohamed Raza

Canada yataifisha ‘dege’ la mizigo la Urusi

Canada yataifisha 'dege’ la mizigo la Urusi

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:9
  • Today's page views 9
  • Total visitors 13,065
  • Total page views 14,810

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In