• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Wabunge watakiwa kuwa mstari wa mbele katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira

by bajeti
June 10, 2023
in Mazingira
0
Wabunge watakiwa kuwa mstari wa mbele katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Khamis Hamza Khamis (kulia) akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi wa Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Sigsbert Kavishe mara baada ya kumalizika kwa semina ya Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria pamoja na Kamati ya Maji na Mazingira iliyofanyika Juni 07, 2023 jijini Dodoma.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,DODOMA

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Khamis Hamza Khamis  amewataka wabunge kuwa mstari wa mbele katika suala zima la uhifadhi na utunzaji wa mazingira.

Mbali na hilo lakini pia wametakiwa  kuhamasisha jamii katika shughuli za upandaji wa miti, utunzaji wa vyanzo vya maji kwani kwa kufanya hivyo kutawezesha kuunga mkono juhudi za serikali katika kusukuma mbele ajenda ya mazingira.

Kauli hiyo imetoa Juni 07, 2023 jijini Dodoma wakati wa kufunga semina kwa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria pamoja na Kamati ya Maji na Mazingira  kuhusu Biashara ya Kaboni.

Amesema Ofisi hiyo itaendelea kutoa semina kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wananchi kuhusu tafsiri na dhana halisi kuhusu manufaa na faida za Biashara ya Kaboni ili kujenga uelewa wa pamoja katika jamii.

“Tumekusudia kutoa mafunzo haya kwa wabunge na wajumbe wa kamati zetu, mafunzo haya yanakuwa endelevu kwani sisi wabunge tuna ushawishi mkubwa katika jamii na tunalosema tunasikilizwa na wananchi” amesema Khamis.

Aidha Khamis amesema katika siku za hivi karibuni kumeibuka maswali kutoka kwa wabunge na wananchi kwa ujumla kuhusu tafsiri na dhana halisi ya biashara hii huku wabunge wengi walipenda suala hili lipatiwe ufafanuzi wa Serikali kuhusu biashara ya kaboni, hivyo kwa kutambua umuhimu huo serikali imeandaa mpango wa mafunzo na semina mbalimbali kwa wabunge.

Awali akizungumza katika semina hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, Jackson Kiswaga ameipongeza Ofisi ya Makamu wa Rais  na kutoa wito wa kuhakikisha kuwa mafunzo hayo yanakuwa endelevu ili kuweza kuwajengea uwezo wabunge.

“Katika hili la Biashara ya Kaboni, naipongeza Serikali kwa hatua hii muhimu tuliyofikia ambayo imelinda zaidi maslahi ya taifa kuhusu rasilimali za misitu.

Hapa kwetu square metre moja ni takribani dola 80 ikilinganisha na Marekani ambapo ni Dola 50 kwa square metre moja, hivyo ni jambo la kujipongeza na tunapaswa kuweza mikakati madhubuti ili tuweze kunufaika” amesema Kiswaga

Aidha, Kiswaga ameiomba Ofisi ya Makamu wa Rais kuweka utaratibu wa usimamizi mahsusi ili kuhakikisha kuwa wananchi wanaozungukwa na rasilimali zitokanazo na Biashara ya Kaboni ikiwemo misitu wananufaika kupitia miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi itakayoibuliwa na wawekezaji.

Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Abdallah Mitawi amesema Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imejipanga kukamilisha utekelezaji wa miradi yote ya mazingira iliyopo pande zote za Muungano ili kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea kunufaika na hivyo kufikia malengo ya miradi hiyo.

“Hivi karibuni tumepata ‘extension’ (kuongezewa muda) katika miradi ya mazingira, hivyo tumejipanga kuhakikisha kuwa miradi yote iliyopo upande wa Tanzania Bara na Zanzibar inakamilika kama ilivyopangwa” amesema Mitawi.

 

 

Next Post
CCM Zanzibar ‘yamlilia’ Mohamed Raza

CCM Zanzibar ‘yamlilia’ Mohamed Raza

Canada yataifisha ‘dege’ la mizigo la Urusi

Canada yataifisha 'dege’ la mizigo la Urusi

Daraja

Daraja

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:9
  • Today's page views 9
  • Total visitors 13,065
  • Total page views 14,810

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In