• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Kaliua kufanya biashara ya Kaboni baada ya kuanzisha misitu ya hifadhi

by bajeti
June 6, 2023
in Mazingira
0
Kaliua kufanya  biashara ya Kaboni baada ya kuanzisha misitu ya hifadhi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Selemani Jafo (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora Dkt.Rashid Chuachua na ujumbewake kuhusu kuanzisha hifadhi ya misitu ili kufanya biashara ya Kaboni Juni 6,2023 jijini Dodoma(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,DODOMA

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora imejipanga kuanzisha mradi wa hifadhi ya misitu kwa ajili ya biashara ya kaboni.

Hayo yamebainika Juni 06, 2023 jijini Dodoma  wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Selemani Jafo alipofanya kikao na Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Dkt. Rashid Chuachua pamoja na ujumbe wake waliomtembelea kwa ili kuwasilisha taarifa ya kusudio la kuanzisha mradi wa hifadhi za misitu kwa ajili ya biashara ya Kaboni.

Akizungumza mara baada ya mkutano huo,Jafo amesema Serikali inaendelea kufungua milango kwa wawekezaji wa Biashara ili kuhifadhi mazingira.

Amesema Ofisi ya Makamu wa Rais ipo tayari kuendelea kutoa elimu kwa umma ili kuwapa uelewa wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini zikiwemo halmashauri kuhusu faida za kupanda miti na kuhifadhi misitu.

“Kutokana na Mikataba ya Kimataifa ya Mabadilkiko ya Tabianchi, sisi kama nchi tumejipanga vizuri kuhakikisha wananchi wanafaidika na biashara hii na ndio maana tumeandaa kanuni na mwongozo,” amesema Jafo.

Aidha ameupongeza uongozi wa wilaya hiyo kwa kuhifadhi misitu na nia yao ya kuwekeza katika biashara ya Kaboni akisema kuwa mbali ya kuhifadhi mazingira lakini pia itakuwa chanzo cha mapato ya halmashauri.

Kwa upande wake Dkt. Chuachua amesema kusudio la kuanzisha mradi wa hifadhi ya misitu kwa ajili ya hewa ya ukaa ni kupata fursa ya biashara hiyo ambayo faida yake itasaidia kuboresha huduma kwa wananchi wake.

Amesema wilaya ina fursa kubwa ya kuwekeza katika biashara hiyo kwa kuzingatia kuwa ina kilomita za mraba 12,084.5 sawa na asilimia 86 ya eneo lote la wilaya hiyo.

“Mradi huu ni muhimu kwani utasaidia kuongeza wigo wa mapato ya halmashauri ambayo kwa asilimia 80 yamekuwa yakitokana na mazao ya kilimo lakini pia utasaidia katika kutunza mazingira ya ardhi oevu ambayo ndio chanzo cha maji katika Mto Malagarasi na Ziwa Tanganyika”amesema Dkt.Chuachua

Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Andrew Komba amebainisha kuwa Biashara ya Kaboni Kimataifa inasimamiwa na Umoja wa Mataifa kwa lengo kuwezesha nchi wanachama kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Dkt. Komba ameongeza  kuwa mabadiliko ya tabianchi yanasababisha ongezeko la joto duniani na vipndi vya baridi na mvua kupungua hali inayochangia ukame hivyo uwepo wa misitu mingi itasaidia katika kunyonya gesijoto inayochangiwa na shughuli za kibinadamu zikiwemo moshi unaotokana na magari na viwanda.

 

 

Next Post
Utafiti:Watoto walionyonya maziwa ya mama hufaulu zaidi shuleni

Utafiti:Watoto walionyonya maziwa ya mama hufaulu zaidi shuleni

Wabunge watakiwa kuwa mstari wa mbele katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira

Wabunge watakiwa kuwa mstari wa mbele katika uhifadhi na utunzaji wa mazingira

CCM Zanzibar ‘yamlilia’ Mohamed Raza

CCM Zanzibar ‘yamlilia’ Mohamed Raza

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In