• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Urusi yaizamisha meli ya kivita ya Ukraine kwa makombora

by bajeti
June 1, 2023
in Habari
0
Urusi yaizamisha meli ya kivita ya Ukraine kwa makombora
Share on FacebookShare on Twitter

MOSCOW,URUSI

WIZARA ya Ulinzi ya Urusi imetangaza kuwa, jeshi la nchi hiyo limeshambulia na kuangamiza meli ya mwisho ya kivita ya Ukraine katika bandari ya Odesa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la habari la IRNA lilinukuu taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Urusi ikisema kuwa, jeshi la anga la nchi hiyo limetumia silaha yenye shabaha ya hali ya juu kuteketeza meli ya mwisho ya kivita ya Ukraine ijulikanayo kwa jina la Yuri Olefirenko katika bandari ya Udesa ya kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Meli ya kivita ya Yuri Olefirenko ilitengenezwa nchini Urusi katika muongo wa 1990 lakini ilikuwa ikimilikiwa na Ukraine baada ya kusambaratika Umoja wa Kisovieti (USSR).

Meli hiyo imefanyiwa matengenezo kwa muda mrefu na matengenezo makubwa zaidi yalifayika mwaka 2016.

Wizara ya Ulinzi wa Urusi  pia imesema katika taarifa yake hiyo kwamba, hivi sasa mapigano makali yanaendelea katika eneo la Avdeevka lililoko katika njia ya kuelekea kwenye jimbo la Donetsk.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, idadi ya wanajeshi wa Ukraine waliouawa katika kipindi cha masaa 24 ya hadi wanatoa taarifa hiyo walikuwa 200.

Tangufebruari 24,2022,Urusi ilidai kuanzisha oparesheni ya kijeshi nchini Ukraine na miongoni mwa maeneo yanayolengwa sana na jeshi la Urusi  ni ya majeshi ya anga na baharini ya Ukraine na kuangamiza zana na vifaa vya majeshi hayo.

Urusi inatumia manuwari zake za kijeshi na makombora yake ya kisasa kuangamiza maeneo ya kijeshi ya serikali ya Kyiv.

 

Next Post
Serikali yawaonya wafanyabishara bidhaa za plastiki

Serikali yawaonya wafanyabishara bidhaa za plastiki

SMZ yawarudisha shule watoto 28,981 walioacha  masomo

SMZ yawarudisha shule watoto 28,981 walioacha masomo

Kaliua kufanya  biashara ya Kaboni baada ya kuanzisha misitu ya hifadhi

Kaliua kufanya biashara ya Kaboni baada ya kuanzisha misitu ya hifadhi

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:6
  • Today's page views 6
  • Total visitors 13,062
  • Total page views 14,807

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In