• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

OUT kuwatumia wahitimu 50,000 kuboresha mitaala yake

by bajeti
June 14, 2023
in Habari
0
OUT kuwatumia wahitimu 50,000 kuboresha mitaala yake

Makamu Mkuu wa chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) Prof. Elifas Bisanda (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Juni 13,2023 jijini Dar es Salaam juu ya kuwatumia wahitimu wao kuboresha mitaala na mifumo inayotumika kufundishia wanafunzi.(Picha na mpigapicha wetu)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

CHUO Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), kimesema kitawatumia  wahitimu wake zaidi ya 50,000 walioko ndani na nje ya nchi ili kuboresha mitaala na mifumo yake itakayoendana na mahitaji ya soko ikiwemo fursa za kuajiri wengine na kujiajiri.

Taasisi hiyo ya elimu ya juu nchini, ambayo ni ya tatu kuanzishwa baada ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine(SUA) cha mkoani Morogoro, imejipanga kuwa kitovu cha elimu inayokwenda na wakati.

Hayo yameelezwa Juni 13,2023 jijini Dar es Salaam na Makamu Mkuu wa chuo hicho (VC), Prof. Elifas Bisanda wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Makao Makuu ya chuo hicho.

Amesema kupitia Mradi wa Mageuzi ya Elimu ya Juu Kiuchumi (HEET), ambao unafadhiliwa na Benki na Dunia, OUT wameamua kuwatafuta wahitimu wote (Alumni) na kupata maoni yao ya kuboresha utoaji wa elimu chuoni hapo.

“Tumeanza kutoa wahitimu wa kwanza mwaka 1999, hadi sasa tuna zaidi ya wahitimu 50,000 kila mahali, lakini tangu tuanze kutoa wahitimu hadi sasa mambo mengi yamebadilika katika dunia.

“Leo tunazungumzia mapinduzi ya nne ya viwanda, ambayo yametawaliwa na akili bandia yaani ‘Artificial Intelligence’ hivyo lazima tukae chini kama wanataaluma, tuone namna bora ya kuendana na mabadiliko haya kwa manufaa ya mhitimu, jamii inayomzunguka na taifa,” amesema Prof.Bisanda.

Prof.Bisanda amebainisha kuwa wameona uhitaji wa kuboresha mitaala na program zao, kutokana na uhalisia uliopo, kwamba mitaani kumejaa wahitimu ambao hawana uwezo wa kufanya kwa vitendo waliyoyasoma darasani lakini wanasubiri kuajiriwa.

Aidha ameongeza kuwa hiyo ndio sababu wanataka kuwafikia wahitimu wa OUT na waajiri ambao wameajiri wahitimu wa chuo hicho, ili kupata maoni yao katika maeneo yote yanayohusiana na kumwandaa mwanafunzi au mwajiriwa kulingana na mazingira ya sasa.

“Tunawaita wanafunzi wetu wa zamani, watupe maoni yao juu ya wapi na kipi tuboreshe, wapi na eneo gani tupunguze, kipi tuondoe, kwa sababu hakuna maana ya sisi tuendelee kutoa programu ambazo mhitimu akimaliza, haajiriki wala hawezi kuajiri wengine,” ameeleza Prof.Bisanda.

Prof. Bisanda ametolea mfano mabadiliko ya nyakati katika programu ya uhasibu, ambayo awali ilihusisha utunzaji wa vitabu vya hesabu na utunzaji wa fedha katika makabati, taaluma ambayo sasa inahitaji mifumo ya kidigitali isiyohitaji vitabu na droo za kutunzia fedha.

Mmoja wa wahitimu wa chuo hicho, Edius Marcel, amesema tayari amekamilisha kujaza utafiti huo na kuwataka wahitimu wenzake ndani na nje ya nchi, kuharakisha jukumu hilo ili kusaidia katika kujenga taasisi imara itakayowaandaa vizuri wanafunzi wa sasa na wa wakati ujao.

OUT kupitia mradi wa HEET, inajenga maabara saba za kisasa za sayansi katika mgawanyo wa kanda nchini,kuwajengea uwezo wahadhiri na wakufunzi wake ikiwemo kuboresha mitaala na kufanya mapitio ya mifumo yake iendane na mahitaji ya wakati.

Next Post
CCM:Wasomi fanyeni utafiti miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali

CCM:Wasomi fanyeni utafiti miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali

Google yaipongeza bajeti.co.tz

Google yaipongeza bajeti.co.tz

Finland kuzinyima misaada nchi za kiafrika zilizogoma kuipinga Urusi

Finland kuzinyima misaada nchi za kiafrika zilizogoma kuipinga Urusi

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In