• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

TPA yapongezwa kulinda mazingira

by bajeti
July 29, 2023
in Mazingira
0
TPA yapongezwa kulinda mazingira

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo (Katikati) akizungumza na viongozi wa TPA mkoani Mtwara juu ya uhifadhi wa mazingira kuhusu makaa ya mawe yanayosafirishwa n kupitia Bandari ya Mtwara Julai 27,2023.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,MTWARA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo ameupongeza uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) mkoani Mtwara kwa kushirikiana na Kampuni ya Ruvuma Coal kwa hatua ya kulinda mazingira.

Hata hivyo Waziri Jafo ameonesha kuridhishwa na uzingatiaji wa Kanuni na Sheria ya Mazingira katika Bandari ya Mtwara.

Pongezi hizo zimetolewa Julai 27,2023 mkoani Mtwara  wakati wa ziara ya kikazi ya Dkt. Jafo ya kukagua shughuli za uhifadhi wa mazingira eneo la utunzaji na usafirishaji wa makaa ya mawe zinazofanyika katika bandari hiyo.

Aidha, Waziri Jafo amesema ameridhishwa na namna ambavyo wameweka uzio kuzunguka eneo yanapohifadhiwa makaa ya mawe ili kudhibiti vumbi lisisambae na kuathiri wananchi.

“Binafsi nikiwa na dhamana ya kusimamia sekta ya mazingira nimeridhika kwani mmetekeleza maelekezo yangu niliyoyatoa nilipofanya ziara katika siku zilizopita,” amesema Dkt. Jafo.

Katika hatua nyingine, Waziri Jafo amewaelekeza wasafirishaji wa makaa ya mawe kuhakikisha malori yanayosafirisha bidhaa hiyo yanafunikwa kwa turubai ili kudhibiti uchafuzi wa mazingira.

Akiwa katika eneo la kuhifadhia makaa ya mawe ya Kampuni ya Jitegemee Holdings, amesema ni lazima malori yote yafunikwe kwa kutofanya hivyo kunasababisha vumbi katika mazingira.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas Ahmed amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu Bandari ya Mtwara kutumika kusafirishia bidhaa ya makaa hayo ya mawe akisema kuwa inaliingizia taifa kipato na kukuza uchumi.

Kuhusu maelekezo yaliyotolewa na Waziri Jafo, Ahmed ameahidi kwa kushirikiana na wataalamu kutoka ofisi yake kuwasimamia wawekezaji ili kuwa na biashara isiyo na madhara kwa wananchi.

Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda ya Kusini Mhandisi Boniphace Guni ameahidi kusimamia agizo hilo ili liweze kutekelezeka kwa muda uliopangwa.

Desemba 20, 2021 Waziri Jafo alifanya ziara bandarini hapo na kutoa muda wa miezi sita kwa uongozi kufanya marekebisho ya dosari za kimazingira zilizobainika ikiwemo kuandaa eneo maalumu lililokidhi vigezo ambalo litatumika kuhifadhi makaa ya mawe yanayosafirishwa.

 

Next Post
Kinana aingilia kati bei ya pamba,uvamizi wa tembo

Kinana aingilia kati bei ya pamba,uvamizi wa tembo

Dkt.Mpango ataka Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) kuvutia washiriki kutoka mataifa mengine

Dkt.Mpango ataka Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) kuvutia washiriki kutoka mataifa mengine

TBA yatakiwa kujenga nyumba zenye ubora na kukidhi mahitaji ya soko

TBA yatakiwa kujenga nyumba zenye ubora na kukidhi mahitaji ya soko

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:5
  • Today's page views 5
  • Total visitors 13,061
  • Total page views 14,806

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In