• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Maafisa Ununuzi na Ugavi wahimizwa kuzingatia sheria

Itasaidia kulinda afya za binadamu na mazingira

by bajeti
February 10, 2024
in Habari
0
Maafisa Ununuzi na Ugavi wahimizwa kuzingatia sheria

Mhandisi Goodluck Rulagora kutoka Chuo cha Uvuvi Bagamoyo (FETA) akitoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya vipimo sahihi vya kemikali vinavyotumika katika vifaa mbalimbali ikiwemo mitungi ya gesi kwa maaafisa ununuzi na ugavi kutoka serikalini wakati wa mafunzo kuhusu utekelezaji wa itifaki ya montreal inayohusu kemikali zinazomong’onyoa tabaka la ozoni Agosti 27, 2023 Jijini Dodoma.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,DODOMA

WATAALAMU wa ununuzi na ugavi Serikalini wamehimizwa kuzingatia miongozo ya Sheria ya Manunuzi ya Umma ili kuepuka manunuzi ya vifaa vyenye ukomo wa matumizi ambavyo husababisha madhara mbalimbali kwa afya ya binadamu na mazingira.

Hayo yameelezwa Agosti 27, 2023 Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Manunuzi na Ugavi wa Ofisi hiyo  Juliana Mkalimoto wakati akifunga warsha ya siku mbili ya mafunzo kwa maafisa ununuzi na ugavi kuhusu utekelezaji wa itifaki ya montreal inayohusu kemikali zinazomong’onyoa tabaka la ozoni.

Amesema maafisa ununuzi na ugavi ni wadau muhimu wanaopaswa kuzingatia utekelezaji wa itifaki ya Montreal kwa kuwa ndio wahusika wakuu wa huduma ya manunuzi wa vifaa na vitendea kazi mbalimbali vinavyotumika na Serikali kupitia Wizara, Idara na Taasisi za umma katika kutekeleza majukumu yake kwa wananchi.

Mkalimoto amesema Serikali imekuwa ikitumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya huduma za ununuzi na ugavi katika utoaji wa huduma, hivyo ni wajibu wa Maafisa ununuzi na ugavi kuzingatia thamani ya fedha wakati wa kushindanisha zabuni mbalimbali.

“Kama mnavyofahamu Serikali inaendelea na ujenzi wa majengo katika maeneo mbalimbali nchini na mfano mzuri ni kule Mtumba (Dodoma),tukiwa kama wataalamu tunapaswa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu wakati wa michakato ya zabuni ili kuepuka uagizaji na uingizaji wa vifaa vyenye ukomo wa matumizi ambavyo vina madhara ya afya kwa binadamu na mazingira” amesema Mkalimoto.

Aidha Mkalimoto amesema kwa kutambua umuhimu wa mafunzo hayo kwa watumishi wa kada ya ununuzi na ugavi, Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imekusudia kutoa mafunzo hayo kwa maafisa ununuzi na ugavi waliopo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Sekretarieri za Mikoa.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Kemilembe Mutasa amesema mafunzo hayo ni moja ya juhudi zinazoendelea kufanywa na Serikali katika kuhakikisha kuwa elimu kuhusu udhibiti wa vifaa vya kemikali inaendelea kutolewa kwa makundi mbalimbali katika jamii.

“Tumepanga mafunzo haya pia yatolewe kwa upande wa Zanzibar kwa kuwa kule kuna bandari ambayo inatumika kuingiza na kupokea bidhaa za aina mbalimbali ikiwemo kemikal,tumekusudia mafunzo haya kuwa endelevu ili tuweze kujenga uelewa wa pamoja kwa jamii” amesema Kemilembe.

Naye Afisa Ununuzi na Ugavi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,  Stanslaus Kagali ameishukuru Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuandaa mafunzo hayo yamewapa uelewa kuhusu umuhimu wa ukomo wa matumizi ya vifaa vyenye kemikali ikiwemo majokofu na ambavyo mara kwa mara vimekuwa vikinunuliwa na Serikali.

“Asilimia 75 ya fedha za Serikali zinahusiana na huduma za ununuzi na ugavi na tunashukuru kupatiwa mafunzo haya kwa kuwa yanatuwezesha kubaini aina ya vifaa ambavyo havifai kwa ajili ya matumizi kutokana na madhara yake kwa afya ya binadamu na mazingira” ameongeza Kagali.

Mafunzo hayo ya siku mbili yameshirikisha jumla ya maafisa ununuzi kutoka Wizara, Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali pamoja na Watoa mada kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (FETA).

Next Post
Magonjwa yatajwa chanzo cha Mbwamwitu  kutoweka

Magonjwa yatajwa chanzo cha Mbwamwitu kutoweka

Mazungumzo

Mazungumzo

Mahakama yasimama kwa muda kuhakiki kitambulisho cha mwandishi

Mahakama yasimama kwa muda kuhakiki kitambulisho cha mwandishi

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:6
  • Today's page views 6
  • Total visitors 13,062
  • Total page views 14,807

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In