NA MIRIAM SARAKIKYA, ARUSHA
SERIKALI kupitia Taasisi ya Utafiti Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) na Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA) zinaendelea na zoezi endelevu la kuwarejesha Mbwa mwitu ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ikiwa ni kuhakikisha kuwa wanyamapori hao wanaendelea kuhifadhiwa katika mfumo _wa ikolojia_ ya Serengeti.
Hayo yamezungumzwa jijini Arusha Agosti 29,2023 na Mtafiti Mkuu na Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti Serengeti Dkt. Emmanuel Masenga wakati wa zoezi la kuwapokea Mbwamwitu zaidi ya 20 waliotoka Hifadhi ya Taifa Mkomazi na kuhamishiwa katika Hifadhi ya Taifa Serengeti kabla ya kuachiwa huru.
Dkt.Masenga amesema kuwa matokeo ya tafiti yanaonyesha kuwa sababu kuu za kutoweka kwa Mbwamwitu katika Hifadhi ya Serengeti ni magonjwa (Rabies and Canine Distemper Virus) na ongezeko la idadi ya Simba na Fisi ikiwemo kuuawa na wananchi wanapotoka nje ya hifadhi.
Aidha, Dkt. Masenga amesema jitihada za Serikali za kuwarejesha wanyamapori hao ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti ni zoezi endelevu na lilianza tangu mwaka 2011 kwa lengo la kuwahifadhi ili kutunza bioanuwai na kuendeleza utalii.
Dkt. Masenga amebainisha kuwa kama inavyofahamika jukumu kubwa la Taasisi ya Utafiti Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) ni kufanya tafiti za wanyamapori, hivyo TAWIRI inaendelea kufanya tafiti za kina za kuhakikisha Mbwamwitu wanaendelea kuhifadhiwa katika mfumo ikolojia wa Serengeti




Discussion about this post