NA MWANDISHI WETU,DODOMA
BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litaanza kujadili Muswada wa Shjeria ya Uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2023 na Muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi wa Mwaka 2023.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa 29 Januari 2024 jijini Dodoma na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa, Ofisi ya Bunge, imeeleza kuwa Mkutano wa 14 wa Bunge la 12 umepangwa kufanyika kwa muda wa wiki tatu kuanzia tarehe 30 Januari hadi tarehe 16 Februari, 2024.
Taarifa hiyo imebainisha kuwa Mkutano huo umeongezewa wiki moja kutokana na uzito wa majukumu yaliyopangwa ikiwemo uzito wa Miswada itakayoshughulikiwa.
‘’Miswada ambayo imepangwa kujadiliwa katika Mkutano huo ni Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2023 na Muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi wa Mwaka 2023.
”Miswada mingine ni Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa wa Mwaka 2023 na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.5) wa Mwaka 2023.”imeongeza taarifa hiyo
Mbali na Miswada hiyo lakini pia Mkutano huo wa Bunge, Kamati za Kudumu za Bunge zitawasilisha taarifa za shughuli zilizotekelezwa na Kamati kwa mwaka 2023.
Aidha, wastani wa Maswali 250 ya kawaida na Maswali 24 ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu yanatarajiwa kuulizwa na Wabunge.




Discussion about this post