• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Siasa

CCM-Zanzibar:ACT-Wazaleno haina hati miliki ya Zanzibar

Haitishwi kujitoa kwao SUK, sio mara ya kwanza kujitoa,vyama vingine kujaza nafasi yao

by bajeti
March 17, 2024
in Siasa
0
CCM-Zanzibar:ACT-Wazaleno haina hati miliki ya Zanzibar

Katibu wa Kamati ya NEC,Idara ya Itikadi,Uenezi na Mafunzo waChama Cha Mapinduzi Zanzibar Khamis Mbeto Khamis

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR.

KATIBU wa Kamati ya NEC,Idara ya Itikadi,Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Khamis Mbeto Khamis amesema Chama cha ACT-Wazalendo hakina hati miliki ya Zanzibar na ikiwa wajitoa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) basi nafasi yao itachukuliwa na vyama vingine

Amesema ACT-Wazalendo wanatakiwa kujua  kuwa CCM na Serikali zake hazitishwi na yeyote iwe mtu,Chama cha kisiasa,kundi,taasisi ya ndani na nje ya nchi na ikiwa watajitoa basi nchi itaendeleza kubaki salama ikiongiozwa na  CCM.

Hayo ameyasema Machi 17,2024 visiwani Zanzibar wakati akitoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali kwa waandishi wa habari waliofika ofisini kwake Kisiwandui.

Amesema Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) haikuundwa kwa matakwa,hisani na ridhaa ya Chama kimoja cha ACT-Wazalendo bali ipo kwa matakwa ya Wananchi waliopiga kura ya maoni ya kukubali wote kupitia kura ya maoni na kwamba hata kujitoa katika Serikali hiyo unafuatwa mfumo ule ule wa kupiga kura ya maoni.

Ameongeza kuwa madai ya ACT-Wazalendo ya kujitoa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) hayana mashiko kwani Serikali hiyo imeundwa kwa nguvu ya kura ya maoni ya Wananchi wote  kupitia mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984.

Mbeto,amefafanua kuwa  ACT-Wazalendo wana ajenda binafsi ya kuirejesha Zanzibar katika machafuko ya kisiasa kutokana na vitendo na kauli zao hizo za vitisho dhidi ya Serikali iliyopo madarani.

”Kama dhamira ya kujitoa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa itatimia litakuwa sio jambo jipya kwani walishawahi kususia vikao vya Baraza la Wawakilishi na  Uchaguzi wa marudio mwaka 2016 na nchi ilipiga hatua kubwa za kimaendeleo bila uwepo wao.

“Kwanza nataka ACT-Wazalendo wajue kuwa CCM na Serikali zake hazitishwi na yeyote iwe mtu,Chama cha kisiasa,kundi,taasisi ya ndani na nje ya nchi tupo imara hivyo waweke maneno ya akiba wasije kujuta juu ya maamuzi yao ya kukurupuka na mihemko ya kisiasa.

”Wajitoe tu vyama vipo vingi wengine watachukua nafasi yao wasijione  wao ndiyo wenye hati miliki ya Zanzibar na nchi itaendeleza kubaki salama na CCM kuendelea kuwa Chama Tawala”amesema Khamis.

Akizungumzia  juu ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ally Mwinyi, ya kuwaita viongozi wa  chama hicho  kuzungumza nao,Khamis amebainisha kuwa  hilo ni jambo la kawaida kwa Rais wa nchi kukutana na watu mbali mbali kusikiliza maoni yao kisha yeye ndo mwenye maamuzi ya kutekeleza kile anachoona kinafaa.

”Vikao vya Rais wa Zanzibar na ACT-Wazalendo vilikuwa vya maridhiano havina uhalali wa kisheria wa kumlazimisha Rais Dk.Mwinyi atekeleze matakwa yao na kwamba kama ipo nyaraka yoyote yenye saini za makubaliano ya pande zote mbili basi zitolewe hadharani kama wanavyotoa madai yao mengine.

”CCM ipo tayari kukaa mezani kusikiliza maoni,ushauri na hoja za Chama chochote cha kisiasa chenye ushauri mzuri wa kuimarisha masuala mbalimbali ya kijamii,kisiasa na kiuchumi”ameongeza Khamis

Next Post
ZAMBIA

ZAMBIA

Mwanga-Tanzania

Mazungumzo

Urusi yaichanganya dunia,EU yasema sasa ni hatari zaidi kuliko awali

Urusi yatangaza rasmi kuwa iko vitani na Ukraine

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In