• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Siasa

Balozi Dkt Nchimbi: Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar(SUK) imeondoa siasa za chuki na uhasama

Asema mlezi hasusi ila mtoto ndio anayesusa

by bajeti
March 25, 2024
in Siasa
0
Balozi Dkt Nchimbi: Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar(SUK) imeondoa siasa za chuki na uhasama

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi,akizungumza na Wazee wa CCM (hawapo pichani) wa mikoa minne ya kichama Unguja katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar Machi 25,20224.(Picha na CCM)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi amesema uwepo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK)umeondoa hali ya siasa za chuki na uhasama mkubwa uliokuwepo kabla ya kufikiwa kwa uamuzi wa kuundwa kwake,

Amesema uamuzi wa kuwepo kwa Serikali hiyo ulizingatia kutanguliza mbele usalama wa maisha ya watu kuliko maslahi ya vyama vya siasa na kwamba CCM itaendelea kutimiza wajibu wake wa kuongoza kwa misingi ya haki na uwajibikaji ili kudumisha umoja na utulivu nchini.

Balozi Dk. Nchimbi amesema hayo Machi 25,2024 wakati akizungumza na Wazee wa Mikoa minne ya CCM Kichama ya Unguja ikiwa ni siku ya pili akiwa kwenye ziara ya kikazi, akitokea Pemba.

Ameongeza kwa  SUK ilikuwa kwa ajili ya usalama wa maisha ya watu, usalama wa Wazanzibar, usalama wa Watanzania kwani maisha ya watu ni muhimu kuliko kitu chochote na waliweka mbele maslahi ya nchi, utulivu na umoja wao na si vyama vya siasa.

“Mnakumbuka wakati fulani nikiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kila siku nenda rudi kwa helkopita kuja Zanzibar. Tulikuwa tunahangaika kuondosha uhasama na chuki. Najua kuna wakati wenzetu wanapata gadhabu na kuzungumza kwa jazba lakini tuendelee kuwavumilia.

‘’Sisi wana CCM tusiende huko hata kidogo. sisi ndiyo Chama tawala sisi ni walezi na  mlezi hasusi,tusiache wajibu wetu wa kulea hata kidogo na kwamba mtoto ndiye anasusa. na katika hili naomba sana wazee wote wa Zanzibar na Tanzania, mniunge mkono,” amesema Balozi Dk. Nchimbi.

Aidha, Balozi Dk. Nchimbi pia amesisitiza msimamo wa CCM kuendeleza kutimiza wajibu wa kipekee wa kuyalinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na misingi yake, akisema kuwa ndiyo yaliyowaweka watu wote kuwa sawa mbele ya sheria na kuondoa kila aina ya ubaguzi, ukiwemo wa matabaka, rangi na hali ya mtu.

“Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yameondoa matabaka yakaleta utu, sote tunaunganishwa na utu wetu, tunao wajibu wa kipekee kuhakikisha tunaendelea kulinda misingi ya Mapinduzi.

‘’Tuko tayari kuendelea kuyalinda hakuna umbo au rangi au hali inampatia haki zaidi mtu mwingine kuliko mwingine na ukifanya ubaguzi wa namna hiyo wewe ni kaburu tena ukaburu hauna rangi”,alieleza Dkt.Nchimbi.

 

 

Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa,amesema CCM inajivunia kwa kuwa na hazina ya Wazee wenye uzalendo,busara,hekima na uwezo wa kushauri mambo mambo mbalimbali yenye manufaa kwa maendeleo ya Chama na Serikali zake kwa ujumla.

Awali Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM Zanzibar Hadija Jabir,aliwasihi Wazee hao kuendeleza utamaduni wa kukosoa,kushauri na kutoa maoni ya kuimarisha CCM pale wanapoona kuna mambo yanaenda kinyume na misingi ya kuanzishwa kwa Chama hicho.

Next Post
Mumbai:Jiji la tatu duniani kukaliwa na  mabilionea wengi

Mumbai:Jiji la tatu duniani kukaliwa na mabilionea wengi

Wenye ulemavu wa miguu sasa kuendesha magari

Utafiti:Asilimia tatu ya kaya za Tanzania ndizo zinazomiliki magari

Ulinzi na Usalama kwa wanafunzi

Ulinzi na Usalama kwa wanafunzi

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In