• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Utafiti:Asilimia tatu ya kaya za Tanzania ndizo zinazomiliki magari

Robo ya kaya zinamiliki baiskeli,12 pikipiki

by bajeti
March 26, 2024
in Habari
0
Wenye ulemavu wa miguu sasa kuendesha magari

Mhandisi Joseph Taifa akiwaonesha waandishi wa habari na watafiti (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam Machi 8,2023 kifaa alichobuni na kukifunga katika gari ili kumsaidia mtu mwenye ulemavu wa miguu kuendesha kwa kutumia mikono.Picha na Goodluck Hongo

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

UTAFITI  wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2022 (DHS-MIS 2022) umebaini kuwa zaidi ya robo ya kaya za Tanzania zinamiliki baiskeli, ikilinganishwa  na asilimia tatu  zinazomiliki gari/malori.

Utafiti huo uliotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) umeonesha kuwa  asilimia 53 za kaya Tanzania zinamiliki ardhi kwa ajili ya kilimo ambapo asilimia 54 ya kaya za Tanzania Bara na asilimia 20 ya kaya za Zanzibar zina miliki ardhi kwa ajili ya kilimo.

‘’Zaidi ya robo (27%) ya kaya za Tanzania zinamiliki baiskeli, ikilinganishwa na asilimia 12 za kaya zinazomiliki pikipiki na asilimia 3 za kaya zinazomiliki gari/malori.

‘’Asilimia 53 za kaya Tanzania zinamiliki ardhi kwa ajili ya kilimo ambapo 54% ya kaya za Tanzania Bara na 20% ya kaya za Zanzibar zina miliki ardhi kwa ajili ya kilimo’’umeeleza utafiti huo

Aidha utafiti huo umefafanua kuwa Kaya za Tanzania zina wastani wa watu 4.5 ambapo  asilimia 29 ya kaya hizo zinaongozwa na wanawake ambapo takribani nusu sawa na asilimia 46 ya watu wote katika kaya hizo ni watoto wa umri chini ya miaka 15.

Awali akizungumzia utafiti huo Machi,13,2024 mkoani Dar es Salaam wakati wa  Mafunzo kwa  Wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) kuhusu Usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 yaliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Mtakwimu Mkuu kutoka NBS Elinzuu Nikodem amesema Utafiti huo umefanyika nchi nzima ikiwemo na  Zanzibar.

Amesema Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2022 (DHS-MIS 2022) ulilenga kutoa takwimu za kufuatilia na kutathmini hali ya afya ya watu nchini Tanzania.

Aidha ameongeza kuwa  Utafiti wa DHS-MIS wa Mwaka 2022 ni wa saba katika mfululizo wa tafiti za kitaifa za kidemografia na afya zilizowahi kufanyika nchini Tanzania tangu mwaka 1991-92.

‘’Lengo la Utafiti huu ni kupata taarifa muhimu kuhusu kiwango cha uzazi, ndoa, kujamiiana, upendeleo wa kuzaa, ufahamu na matumizi ya njia za uzazi wa mpango, unyonyeshaji watoto wadogo, lishe, vifo vya watoto wadogo na vifo vitokanavyo na uzazi,

‘’ Huduma wakati wa ujauzito na huduma za watoto, malaria, na taarifa nyingine zinazohusu afya, pamoja na kiwango cha malaria kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano’’amesema Nikodem

Next Post
Ulinzi na Usalama kwa wanafunzi

Ulinzi na Usalama kwa wanafunzi

Uchumi wa Tanzania kukua kwa asilimia sita

Uchumi wa Tanzania kukua kwa asilimia sita

Jamii yatakiwa kusaidia watoto yatima na wenye uhitaji maalum

Jamii yatakiwa kusaidia watoto yatima na wenye uhitaji maalum

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:9
  • Today's page views 9
  • Total visitors 13,065
  • Total page views 14,810

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In