• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Jamii yatakiwa kusaidia watoto yatima na wenye uhitaji maalum

by bajeti
April 9, 2024
in Habari
0
Jamii yatakiwa kusaidia watoto yatima na wenye uhitaji maalum

KATIBU wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Bananga (wa nne kutoka kulia) akiwa na viongozi pamoja na watoto yatima wanaolelewa katika Kituo cha Kituo cha Mwandaliwa Orphanage Cente kilichopo mkoani Dar es Salaam Aprili 8,2024.(Picha na Andrew Chale)

Share on FacebookShare on Twitter

NA ANDREW CHALE

KATIBU wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Bananga amesema ni muhimu kusaidia jamii hususani kundi la watoto yatima na wale  wenye uhitaji maalum kwa kuwa hakuna mzazi anayejua kesho yake itakavyokuwa..

Amesema ni muhimu kuendeleza utamaduni huo ndani ya jamii kwa kuwa mzazi anaweza kufurahia kuwa na mtoto au watoto wake sasa hivi  lakini hajui yajayo ambapo anaweza kufariki dunia na kuwaacha  yatima

Bananga ameyasema hayo Aprili 8,2024 mkoani Dar es Salaam wakati wa hafla  maalum ya utoaji wa msaada kwa watoto yatima wa Kituo cha Mwandaliwa Orphanage Cente iliyoandaliwa na Taasisi ya Hitinas Foundation.

“Ukimsaidia mtoto yatima unaweka hazina nzuri mbele ya Mwenyezi Mungu, ambayo itakusaidia wewe au kizazi chako katika siku zijazo.

‘’Hongereni sana. (Hayati) Mzee Ali Hassan Mwinyi Rais wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema (katika maisha yako) jiandae uwe hadithi nzuri huko mbeleni kwa hiyo mlichofanya Hitinas Foundation kupitia Mkurugenzi, nimefurahia sana, kwa sababu futari hii ya leo tumekula na wanaostahili kabisa”amesema Bananga

Bananga ameongeza kuwa milango ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam ipo wazi na wako tayari kutoa ushirikiano watakaouhitaji ili kuwafanya watoto hao kuishi katika mazingira kama walivyo watoto wengine kwenye familia zao.

‘’Msikwazike wakati mnafanya mambo yenu,kwa haya ya kusaidia jamii njooni, kwa maana sisi wote nyumbani kwetu tuna mayatima watarajiwa leo tupo mambo yanaenda sawa sawa lakini kesho hatupo”amesisitiza Bananga’’

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Hinatas Foundation, Ayshat Sanya amesema walidhamiria kufutarisha watoto 105 wa kituo hicho ikiwemo kukusanya fedha kwa ajili ya kuwanunulia mahitaji mengine kama nguo na viatu vya kusherehekea sikukuu ya Eid.

.‘’Tunaishukuru jamii yetu, sisi ni taasisi inayosaidia jamii na asilimia 100 ni taasisi isiyojitengenezea faida na tumeweza kupata Tsh. Mililioni . tatu za nguo za Eid, ambapo tutanunua na kuwasilisha kituoni.

‘’Kituo cha Mwandaliwa leo ni mara ya kwanza tumeanza nao na tumeahidi kuendelea kuwashika mkono lakini tumeshafanya hivi na kituo kingine  cha Al Madina  na tutaendelea kushirikiana na vituo vingine pia’’ amesema Sanya

Naye Mlezi wa Mwandaliwa Orphanage Center ambaye pia ni Afisa, Elimu wa kituo hicho, Omary Daudi ameushukuru uongozi wa Hinatas Foundation kwa kuwaunga mkono katika kusaidia watoto hao.

”Watoto wamefurahi mno kwa tukio hili,lakini tunapoondoka hapa bado tuna mahitaji mengine mbalimbalii kama vyakula, sare za shule, sasa tuna usafiri changamoto ni fedha kwa ajili ya mafuta ya kuweka hivyo tunapenda kuona wadau mbalimbali wakiendelea kujitokeza kutusaidia” amebainisha Daudi.

Aidha, amebainisha kuwa, kituo hicho kina jumla ya watoto 105 kati yao wa kike ni 50 na wa kiume ni 55.

Next Post
Mvua zasababisha vifo vya watu 15 wakiwemo watoto 12

Mvua zasababisha vifo vya watu 15 wakiwemo watoto 12

TCB kutoa mikopo ya Sh.Bilioni 300

TCB kutoa mikopo ya Sh.Bilioni 300

Rais Samia ashiriki ibada ya Eid El Firti

Rais Samia ashiriki ibada ya Eid El Firti

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:6
  • Today's page views 6
  • Total visitors 13,062
  • Total page views 14,807

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In