• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Wakili Mchau:Mahakama za Tanzania ni za sheria

Unaposema hujatendewa haki ni lazima useme sheria gani haikufuatwa

by bajeti
May 7, 2024
in Habari
0
Wakili Mchau:Mahakama za Tanzania ni za sheria

Wakili kutoka Kampuni ya Uwakili ya Mchau and Co.Advocates,Hardson Mchau akiwa katika shughuli zake za utetezi mahakamani

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

WATANZANIA wametakiwa kufahamu kuwa Mahakama nchini zinatoa maamuzi kwa mujibu wa sheria na sio kwa misingi ya maelezo au maneno.

Ufafanuzi huo umetolewa na Wakili kutoka Kampuni ya Uwakili ya Mchau and Co.Advocates,Hardson Mchau wakati akizungumza na Bajeti Mei 6,2024 jijini Dar es Salaam kuhusu baadhi ya watu kulalamikia maamuzi ya mahakama yanayoupa ushindi upande wa pili na kueleza kuwa hawakutendewa haki.

Mchau amesema Mahakama ndio chombo kilichopewa Mamlaka ya Utendaji wa Haki Tanzania na kwa kuwa ndio chombo cha kutenda haki wanaamini kuwa Mahakama huwa inatenda haki.

Amesema mtu yeyote anayelalamika kuhusu mahakama kutotenda haki anatakiwa alalamike kwa misingi ya kisheria na sio misingi ya maelezo au maneno na anaposema hajatendewa haki ni lazima afafanuwe kuwa ni sheria gani haikufuatwa.

”Watu hawajui kuwa mahakama ni mahakama ya sheria,hapo ndio watu wanashindwa kujua tofauti ya haki na sheria.

”Hizi ni Mahakama za Sheria na Mahakama za Haki zipo ambazo zinaweza zisiangalie Sheria lakini kwa Tanzania Mahakama zetu ni Mahakama za Sheria na zinaitwa Court of Law.

”Sisi mahakama zetu ni mahakama za sheria na tunaangalia sheria inasemaje na ndio hivyo maamuzi  yanaenda kutoka kwa mujibu wa sheria.”amesema Mchau

Mchau ambaye ni Mwanachama wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) tangu 2018,amefafanuwa kuwa haki nchini Tanzania inapatikana kwa mujibu wa sheria hivyo wakati mwingine  mtu anahisi ana haki kumbe sheria imemnyima na ndio maana baadhi ya watu wanalalamika kwamba hawakutendewa haki.

”Sisi tunaamini kuwa Mahakama  inatenda haki kwa sababu inafanya kazi kwa mujibu wa sheria na maamuzi yote ya Mahakama yanafanywa kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

”Kwa anayelalamika anatakiwa alalamike kwa misingi ya kisheria na sio misingi ya maelezo au maneno na unaposema hujatendewa haki ni lazima usema sheria gani haikufuatwa na sio kusema kwamba Mahakama haitendi haki”amebainisha Mchau.

Kwa upande wa kukata rufaa,Mchau ameongeza kuwa haki ya kukata rufaa ni haki ya kikatiba kwa kila upande na mtu yeyote ambaye anahisi hajaridhika na uamuzi kuna taratibu za ukataji wa rufaa.

”Je unatakiwa ujiulize hilo shauri lako unaweza kulikatia rufaa?kwa sababu rufaa sio haki ya moja kwa moja lazima ufuate taratibu na sio kila kesi inaweza kukatiwa rufaa kwani zingine rufaa zimezuiliwa kwa mujibu wa sheria”amebainisha Mchau

Amefafanuwa kuwa ikiwa upande wa pili wanaona hawajaridhika na wanahisi wana haki ya kukata rufaa wanaweza kukata rufaa.

Next Post
TMDA:Waandishi andikeni habari za Dawa, Vifaa Tiba na Bidhaa za Tumbaku zenye kuleta tija kwa jamii

TMDA:Waandishi andikeni habari za Dawa, Vifaa Tiba na Bidhaa za Tumbaku zenye kuleta tija kwa jamii

Tunapanda miti

Tunapanda miti

DC Nassari awataka vijana kusoma kwa bidii kufikia malengo yao

DC Nassari awataka vijana kusoma kwa bidii kufikia malengo yao

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:0
  • Today's page views 0
  • Total visitors 13,056
  • Total page views 14,801

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In