• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Marafiki wa Serengeti Uswisi watoa vifaa vya zaidi ya Sh.Milioni 40 kwa TAWA kulinda rasilimali za wanyamapori

by bajeti
June 11, 2024
in Mazingira
0
Marafiki wa Serengeti Uswisi watoa vifaa vya zaidi ya Sh.Milioni 40 kwa TAWA kulinda rasilimali za wanyamapori

Askari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) wakifunga moja ya mahema yaliyotolewa na Marafiki wa Serengeti Uswisi Juni 9,2024 jijini Arusha.(Picha na TAWA)

Share on FacebookShare on Twitter

NA BEATUS MAGANJA,ARUSHA .

MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imepokea vifaa vya aina mbalimbali kutoka kwa Marafiki wa Serengeti Uswisi vyenye thamani ya zaidi ya Sh.Milioni 40 ili vitumike katika kusaidia  kuhifadhi na kulinda rasilimali za wanyamapori.

Hata hivyo ufadhili huo wa vifaa vya doria kwa TAWA umetolewa ili  kuunga mkono jitihada za Serikali za kuhifadhi na kulinda rasilimali za wanyamapori nchini ikiwa ni pamoja na  udhibiti wa wanyamapori  wakali na waharibifu,

Vifaa vilivyotolewa na  Marafiki wa Serengeti Uswisi “Friends of Serengeti Switzerland” ni pamoja na  mahema, mabegi ya kulalia “Sleeping bags”   pamoja na Lita 2,120 za mafuta ya gari kwa ajili ya kusaidia shughuli za doria kwa Askari wa TAWA Kanda ya Kaskazini.

Akikabidhi vifaa hivyo Juni 9,2024 katika Ofisi za TAWA Kanda ya Kaskazini  zilizopo jijini Arusha  kwa niaba ya Bodi ya Marafiki wa Serengeti Uswisi, Suzan Shio amesema lengo na shabaha yao ni kusimamia uhifadhi wa mazingira na wanyamapori ili kuhakikisha Tanzania inakuwa katika hali yake ya uasili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.

“Tumekuwa tukifanya shughuli za ufadhili wa uhifadhi kwa miaka kadhaa nchini Tanzania, na kwa TAWA tumeanza zaidi ya miaka 10 iliyopita (tangu ikiwa Idara ya Wanyamapori) na  hasa tulijikita kwenye ufadhili wa mafuta kwa ajili ya kuwasaidia askari kufanya doria” amesema Shio

Shio  ameishukuru TAWA kwa ushirikiano inayoendelea kuutoa kwa wadau hao na kukiri kuwa ushirikiano huo umekuwa chachu ya kuwapa moyo wa kuendelea kuwafadhili.

Kaimu Kamanda wa Uhifadhi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori TanzaniaTAWA Kanda ya Kaskazini Privatus Kasisi akipokea vifaa mbalimbali vya kulinda na kuhifadhi rasilimali za wanyamapori kutoka mwakilishi wa Bodi ya Marafiki wa Serengeti Uswisi, Suzan Shio Juni 9,2024 jijini Arusha.(Picha na TAWA

Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo, Kaimu Kamanda wa Uhifadhi TAWA Kanda ya Kaskazini Privatus Kasisi ameishukuru bodi ya Marafiki wa Serengeti kwa ufadhili huo ambao unalenga kuboresha  usimamizi wa shughuli za uhifadhi na ulinzi wa rasilimali za wanyamapori hususani katika kukabiliana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu katika Kanda hiyo.

“Sisi kama TAWA tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa bodi ya Marafiki wa Serengeti Uswisi ambao wamekuwa wakitusaidia misaada mbalimbali kwa ajili ya kusimamia uhifadhi na ulinzi wa rasilimali za wanyamapori kwa muda mrefu na wamekuwa wakitupa mafuta, mahema na viona mbali “binoculars’’

‘’Kanda ya Kaskazini inasimamia maeneo makubwa yanayounganisha  mikoa minne ya Manyara, Arusha, Tanga na Kilimanjaro ambayo yamekuwa yakikumbwa na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu,hivyo kwa kupatiwa msaada huu hususani mahema yatawasaidia sana askari kufanya kazi zao ipasavyo hasa kwa kazi za dharura zinazojitokeza mara kwa mara na kuwalazimu kwenda maeneo ambayo hayana vituo vya kudumu vya askari’’ameongeza Kasisi.

Kasisi  ameiomba bodi hiyo kuendelea kuisaidia TAWA hususani katika Kanda hiyo kwa kuwa wanasimamia maeneo makubwa yenye changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu na uhitaji bado ni mkubwa.

Next Post
TANROADS:Ujenzi wa BRT hautaathiri sanamu la askari  lililopo Posta-Dar es salaam

TANROADS:Ujenzi wa BRT hautaathiri sanamu la askari lililopo Posta-Dar es salaam

TAWA:Tumedhibiti utoroshwaji wa Nyara za Serikali katika Uwanja wa Ndege JNIA

TAWA:Tumedhibiti utoroshwaji wa Nyara za Serikali katika Uwanja wa Ndege JNIA

TAWA:Tumedhibiti utoroshwaji wa Nyara za Serikali katika Uwanja wa Ndege JNIA

Bodi ya TAWA kupeleka wanyamapori hai Hifadhi ya Pande

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In