• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Monday, May 25, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

LATRA ‘yapata dawa’ kwa daladala zinazokatisha njia

by bajeti
July 8, 2024
in Habari
0
LATRA ‘yapata dawa’ kwa daladala zinazokatisha njia

Mkurugenzi wa Udhibiti Usafriri wa Barabara (LATRA) DCP Johansen Kahatano akizungumza na waandishi wa habari Julai 7,2024 mkoani Dar es Salaam juu ya mfumo wa kufuatilia daladala wakati wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea mkoani Dar es Salaam(Picha na bajeti.co.tz)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini  (LATRA) itafunga mfumo maalum wa kufuatilia mwenendo wa gari kwa mabasi yanayotoa huduma ya usafiri ili kudhibiti ukatishaji wa njia zao.

Mbali na kufunga mfumo huo lakini pia ipo katika hatua za maandalizi ya kuweka mfumo wa tiketi zote za daladala kutumia mfumo wa kieletroni.

Kauli hiyo ya imetolewa Julai 7,2024 na Mkurugenzi  wa Udhibiti Usafiri wa Barabara kutoka LATRA DCP Johansen Kahatano wakati wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoeendelea mkoani Dar es salaam wakati akizungumza na Bajeti Communication.

Amesema wanaipongeza Serikali kwa uwekezaji wa barabara hasa za vijijini hivyo kumesaidia kuanzishwa kwa njia mpya nyingi na kufungwa kwa mfumo huo wa uthibiti katika daladala utasadia kuondoa hali hiyo ya ukatishaji wa njia kwa daladala.

‘’Hadi kufikia mwezi Desemba mfumo huo utakuwa umeshafungwa kwa daladala zote lakini pia tunaendelea na uwekaji wa mifumo ili tiketi zote za daladala zitolewe kwa njia ya mtandao.

‘’Lengo ni kuthibiti mapato ya Serikali,mmiliki wa gari na madereva akiwemo na Kondakta wake ambao wataajiriwa rasmi.

‘’Kwa upande wa Mabasi Yaendayo Kasi (BRT) wasafiri watatumia kadi kukata kitiketi zao kama ilivyo eneo la Feri jijini Dar es Salaam kwa watu wanaovuka kuelekea Kigamboni  hivyo hakutakuwa na mfumo wa sasa kila atakayepanda itamlazimu kuwa kadi’’amesema Kahatano

Akizungumzia kuunganisha daladala au mabasi yanayotoka mkoa mwingine na Mkoa wa Dar es Salaam,Kahatano amefafanua kuwa wao wameona sio vibaya kuongeza kilomita tatu au mbili kwa maeneo yaliyopo karibu na yenye muingiliano mkubwa wa watu kuunganisha gari moja kwa kuwa Tanzania ni moja.

Kwa upande wa changamoto wanazokabiliana nazo kwa sasa ni ukatishaji wa safari kwa daladala na ndio maana wamekuja na mfumo huo wa kulifuatilia gari.

‘’Tunatoa wito kwa wananchi wote LATRA imeweka namba pembeni ya daladala na mabasi,hivyo wazitumie kuwapigia ili kutoa taarifa na wao watazifanyia kazi mara moja”amesema Kahatano

Next Post
Tani dawa za kulevya ‘zautikisa’ mwaka 2023.

Tani dawa za kulevya ‘zautikisa’ mwaka 2023.

Kigoma-Tanzania

Kigoma-Tanzania

TARI yagundua mbegu mpya 16

TARI yagundua mbegu mpya 16

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:0
  • Today's page views 0
  • Total visitors 16,454
  • Total page views 18,665

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In