NA MWANDISHI WETU
WANAWAKE zaidi ya 800 wamekamatwa nchini wakituhumiwa kwa kosa la kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Wanawake hao wamekamatwa kwa kujihusisha na biashara za bangi,mirungi,heroin,cocaine na dawa mpya aina ya methamphetamine kwa mwaka 2023 pekee.
Hata hivyo licha ya Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya Mwaka 2015 kutoa hukumu ya kifungo kisichopungua miaka 30 kwa kulima bangi au mirungi na kifungo kisichopungua miaka 30 kwa kufanya biashara ,kusafirisha au kukutwa na heroin,methamphetamine au cocaine isiyozidi gramu 200 na kifungo cha maisha ikizidi gramu 200 wanawake hao wameonekana hawaogopi.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya ya Mwaka 2023 iliyotolewa Mwezi Mei,2024 na Ofisi ya Waziri Mkuu na Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imeeleza kuwa operesheni na ukamataji uliofanyika mwaka 2023 ulifanikiwa kukamata dawa za kulevya za mashambani aina ya bangi na mirungi pamoja na dawa za viwandani aina ya heroin,cocaine,methamphetamine na dawa tiba zenye asili ya kulevya.
Taarifa hiyo iliyosaniwa na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera,Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)Aretas Lyimo imeeleza kuwa jumla ya tani 1965.34 za dawa za kulevya zilikamatwa kwa mwaka 2023 pekee ikiwa ni karibu mara saba zaidi ya kiasi kilichokamatwa tangu Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ianzishwe mwaka 2017.
”Katika mwaka 2023 kiasi cha tani 1757.56 za dawa za kulevya aina ya bangi kilikamatwa kikihushisha watuhumiwa 8,803 kati yao wanaume 8,180 na wanawake 623.
”Mirungi ni dawa ya kulevya ya mashambani ambayo pia imeendelea kuwa tatizo kwa mwaka 2023,jumla ya tani 202.74 ya dawa hii zilikamatwa zikihusisha watuhumiwa 1,179 na kati ya hao wanaume 996 na wanawake 183.
”Mwaka 2023 jumla ya tani 1.31 za dawa za kulevya aina ya heroin ilikamatwa nchini ikihusisha watuhumiw 196 kati ya hao wanaume 168 na wanawake 28”imeleeza taarifa hiyo.
Kwa upande wa dawa za kulevya aina ya cocaine,imefafanuwa kuwa operesheni zilizofanyika mwaka 2023 zilifanikiwa kukamatwa kwa kilo 3.04 za cocaine pamoja na watuhumiwa 32 kati yao wanaume 31 na mwanamke mmoja
‘’Mwaka 2023 jumla ya tani 2.4 za dawa za kulevya aina ya methamphetamine inayotengenezwa kwa kutumia kemikali bashirifu ilikamatwa nchini ikihusisha watuhumiwa tisa katika yao wanaume watano na wanawake wanne’’imeongeza taarifa hiyo.
Hata hivyo sheria Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya Mwaka 2015 inatoa hukumu ya kifungo cha miaka mitatu au faini ya kuanzia Sh.500,000na isiyopungua Sh.1,000,000 au vyote kwa pamoja kwa kutumia dawa za kulevya.
DCEA inapaswa kupongezwa kwa kazi kubwa iliyoifanya kwa mwaka 2023 na jamii kuipa ushirikiano wa hali juu ili kutokomeza biashara hiyo na hali ingekuwaje ikiwa tani hizo na watuhumiwa hao wasingekamatwa.




Discussion about this post