• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Meja Jenerali Mstaafu Semfuko:Watanzania changamkieni fursa ya ufugaji wanyamapori

by bajeti
July 15, 2024
in Mazingira
0
Meja Jenerali Mstaafu Semfuko:Watanzania changamkieni fursa ya ufugaji wanyamapori

Menyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis Semfuko akiwasili katika Banda la TAWA Julai 13,2024 katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) mkoani Dar es Salaam.

Share on FacebookShare on Twitter

NA BEATUS MAGANJA

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Nchini (TAWA) Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis Semfuko amewahimiza watanzania kuchangamkia fursa za ufugaji wa wanyamapori zinazopatikana katika mamlaka hiyo.

Meja Jenerali Mstaafu Semfuko ameyasema hayo Julai 13, 2024 alipotembelea Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii Katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ambayo ni siku ya mwisho mwa maonesho hayo kwa Mwaka 2024.

Aidha Meja Jenerali (Mstaafu) Semfuko amesema ili watanzania waweze kupata kitoweo cha nyamapori kwa urahisi wanapaswa kuingia katika biashara ya ufugaji wa wanyamapori na kwakufanya hivyo wataziwezesha bucha za wanyamapori kufanya kazi vizuri.

Amebainisha kuwa TAWA ina mipango mingi ya kuhakikisha  inapata wawekezaji wakubwa na wadogo ili wawekeze katika maeneo mbalimbali inayoyasimamia kama vile kuwekeza katika mahoteli, vitalu vya uwindaji wa kitalii na ranchi za wanyamapori ili kuongeza idadi ya wanyama hao.

“Sehemu kama Afrika ya Kusini ufugaji wa wanyamapori ni mkubwa sana, kwahiyo mimi natoa rai kwa wananchi hasa watanzania kuingia katika biashara hiyo ya ufugaji wa wanyamapori” amesema Meja Jenerali Mstaafu Semfuko

Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba)yenye kauli mbiu “Tanzania ni Mahali Sahihi pa Biashara na Uwekezaji” yalianza Juni 28, 2024 na kuzinduliwa  rasmi Julai 03, 2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi ambapo yamefungwa rasmi Julai 13, 2024 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dkt. Hussein Ali Mwinyi

 

 

Next Post
Rais Samia:Kilio cha wakulima kudhulumiwa hakipo tena

Rais Samia:Kilio cha wakulima kudhulumiwa hakipo tena

Mahakama yasimama kwa muda kuhakiki kitambulisho cha mwandishi

Mapya yaibuka kesi ya Lydia Lugaga dhidi ya Damas Ndumbaro

RUKWA GIRLS

Rais Dkt.Samia:Amani,utulivu na usalama tulionao ni kwa sababu walimu mnatengeneza watu wazuri

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:17
  • Today's page views 17
  • Total visitors 13,276
  • Total page views 15,024

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In