• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Sunday, January 18, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Rais Samia:Kilio cha wakulima kudhulumiwa hakipo tena

by bajeti
July 15, 2024
in Mazingira
0
Rais Samia:Kilio cha wakulima kudhulumiwa hakipo tena

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan akisikiliza maeleo kutoka kwa Wziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati wa uzinduzi wa vihenge vya kuhifadhia chakula mkoani Katavi Julai 14,2024

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,KATAVI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema bajeti iliyopitishwa na Bunge kwa mwaka wa fedha 2024/25 ni Trilioni 1.25 kutoka Bilioni 460 miaka ya nyuma lengo likiwa ni kumuinua mkulima.

Rais Samia amebainisha kuwa kwa sasa Tanzania inahama kutoka katika kulima na kula na kuelekea katika Kilimo cha biashara.

Rais Samia ametoa kauli hiyo mkoani Katavi Julai 14,2024 wakati akihitimisha ziara yake kwa kutembelea maghala ya kuhifadhi chakula.

Amesema mahindi mpunga mbaazi na mazao yote ya chakula yamekuwa mazao ya biashara  na ndio mazao yanayofanya vizuri katika kujenga uchumi.

”Tumedhamiria kukuza kilimo na tumeweza kuongeza bajeti ya Kilimo kutoka Sh.Bilioni 460 huko nyuma na mwaka huu bajeti ya Kilimo iliyopitishwa na Bunge ni Trilioni 1.25

”Lakini fedha hizi zinakwenda kwenye maeneo kadhaa ya kujenga skimu ya umwagiliaji maji,maeneo ya kukuza huduma za ugani na kama mnavyojua tunatoa mbolea ya ruzuku,Serikali inabeba nusu gharama na mwananchi unalipa nusu gharama ili kukuza uzalishaji zaidi na kuwa na mazao mengi zaidi.

”Tumeanza kufanya biashara na nchi jirani,na sasa hivi tunafanya biashara na Zambia wanachukua zaidi ya tani 600,000 kutoka Tanzania kwa sababu wao wamepata ukame,sasa lazima tukuze tija na uwezo wa maghala yetu ichukule chakula kingi zaidi.”amesema Rais Samia

Amebainisha kuwa kwa sasa wanajipanga ili waweze kufikia tani milioni tatu itakapofika mwaka 2030 kwa Tanzania yote iweze kuhifadhi tani milioni tatu.

‘’Jana nilitoa ruhusa Mkoa wa Katavi iwe Kanda inayojitegemea peke yake katika manunuzi ya nafaka na katika uhifadhi wa chakula na tujielekeze kwenye uzalishaji ili mkulima anufaike na Serikali inufaike na Taifa kwa ujumla linufaike”amesema Rais Samia

Aidha Rais Samia  amebainisha kuwa Sh.Bilioni 14 zimetumika katika mradi huo na kwa sababu wameamua Katavi iwe Kanda inayojitegemea peke yake ni lazima waongeze uwezo wa kuhifadhi

”Kile kilio cha wakulima  cha kudhulumiwa sifa ya mazao yake au grade ya mazao yake au uzito sasa hakipo tena

”Kuna mfumo mzuri wa mkulima wa kupima mazao yake na anaridhika na ni automatic na hauingii mkono wa mtu,unachokiweka ndicho kinachojiandika kwenye mizani”amefafanuwa Rais Samia

Rais Samia ameongeza kuwa wamekusudia kuipandisha NFRA kiutendeaji,kiteknolojia,kifedha na kuwataka wakulima kulima kwa wingi ili anayenunua kwa mkulima anunue kwa haki na vizuri na anayeongeza dhamani ya mazao aongeze vizuri akiwemo na anayeuza naye auze vizuri

Next Post
Mahakama yasimama kwa muda kuhakiki kitambulisho cha mwandishi

Mapya yaibuka kesi ya Lydia Lugaga dhidi ya Damas Ndumbaro

RUKWA GIRLS

Rais Dkt.Samia:Amani,utulivu na usalama tulionao ni kwa sababu walimu mnatengeneza watu wazuri

Maelfu ya wananchi wa Rukwa  walivyomlaki Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan

Maelfu ya wananchi wa Rukwa walivyomlaki Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:27
  • Today's page views 27
  • Total visitors 13,184
  • Total page views 14,930

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In