• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Sunday, May 3, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Makala

NHC yaendelea kuondoa changamoto za makazi Jiji la Kibiashara Dar es Salaam

Mradi wa 711 Kawe wenye nyumba 422 kukamilika April 2026

by bajeti
August 12, 2024
in Makala
0
NHC yaendelea kuondoa changamoto za makazi Jiji la Kibiashara Dar es Salaam

Mradi wa 711 Kawe Residence Kinondoni Dar es Salaam

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

UFUFUAJI wa Mradi wa Kawe katika Manispaa ya Kinondoni ndani ya Jiji la Kibiashara Dar es Salaam nchini Tanzania ni hatua muhimu katika kushughulikia changamoto za makazi zinazowakabili wakazi wa jiji hilo kwa ujumla.

Baada ya kusimama kwa zaidi ya miaka sita, mradi huo muhimu sasa unaendelea kutokana na dhamira thabiti ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Uongozi Madhubuti wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Juhudi za NHC zinaelekea kubadilisha mandhari ya makazi, kutoa nafuu na fursa kwa maelfu ya wakazi, na kuboresha hadhi ya wakazi watakaopata fursa ya kuishi kwenye makazi hayo.

Maendeleo na Uwekezaji Mradi wa Kawe unaoendelea kwa kasi na unaooneka kuahidi kutoa suluhisho la kisasa na nafuu la makazi, hivyo kuboresha hali ya maisha kwa wakazi wake.

Mradi huo utasaidia kupunguza upungufu wa nyumba, kupunguza msongamano, na kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya eneo hilo.

Mradi huo pia utasaidia  jamii kupata manufaa makubwa kutoka kwa miundombinu iliyoboreshwa, hali bora za kuishi, na ongezeko la thamani ya mali ambalo mradi huo utaleta.

Lengo kuu la NHC ni kuhakikisha upatikanaji wa makazi bora kwa Watanzania ambapo pia majukumu mengine ya  shirika hilo ni pamoja na kujenga nyumba za makazi na majengo mengine kwa ajili ya kuuza, kujenga majengo kwa ajili ya miradi rasmi, kutoa vifaa vya ujenzi, kusimamia biashara ya nyumba na majengo, na shughuli nyingine zilizoidhinishwa na Serikali.

Wakati NHC ikiendelea kupambnana na changamoto hizo,makazi yameonekana kuwa  ni hitaji muhimu kwa binadamu na huleta upendo, tumaini, na ndoto zinazotimia.

Nyumba za makazi zinaweza kuwa za kupanga au za kujenga, ambapo mhusika ana mamlaka kamili.

Hata hivyo Watanzania wengi wanaishi katika nyumba za kupanga kutokana na tofauti za kipato na hali ya maisha ambapo baadhi ya nyumba hizo za kupanga zimekuwa na changamoto mbalimbali,ikiwemo kutokaa kwa muda mrefu na kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

NHC imekuwa suluhisho kwa upatikanaji wa nyumba bora za kupanga kwa haraka, rahisi, na gharama nafuu.

Mradi wa 711 Kawe Residence

Tanzania imepiga hatua kubwa katika Sekta ya Ujenzi, hasa mkoani Dar es Salaam ambapo kuna majengo makubwa na ya kisasa.

Miongoni mwa miradi inayojenga sura mpya ya Tanzania ni Mradi wa 711 Kawe Residence, unaomilikiwa na NHC.

Mradi huu wa makazi, unaojulikana

kama (711) Seven Eleven Kawe Residence na unajumuisha nyumba 422 za kuuzwa zilizopo kwenye majengo nane yenye ghorofa 18 kila moja, zikiwa katika eneo la Kawe Manispaa ya Kinondoni,Dar es Salaam.

Mradi wa 711 Kawe unaofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)

Asili ya Jina  (711);Seven Eleven

Jina la Mradi huo,711 Kawe Residence limetokana na viwanja vya awali vya NHC vilivyokuwa vinamilikiwa kama namba 711 na 712.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendeleza kwa kasi mradi huo wenye thamani ya Sh.Bilioni 169.9.

Maendeleo ya Ujenzi

Mradi ulianza rasmi Novemba 2014, lakini ulisimama mwaka 2018,hata hivyo, kutokana na jitihada za Rais Dkt.Samia, NHC ilipewa ruhusa ya kukopa ili kuendeleza mradi huo.

Ujenzi,unaendelea kwa sasa na unatarajiwa kukamilika Aprili 2026 kwa gharama ya Sh.Bilioni 169.9.

Huduma na Vifaa vya Kisasa

Mradi huo unajumuisha nyumba za aina nne ambavyo ni ya  vyumba viwili kawaida (24),Vyumba vitatu kawaida (254),Vyumba vitatu vya kifahari (128) na Vyumba vinne vya kifahari (16) huku kila nyumba ikijitosheleza kwa huduma muhimu kama sebule, eneo la kulia chakula, maliwato ya wageni, na jiko kubwa la kisasa.

Pia, kuna maegesho ya magari, sehemu za michezo, maeneo ya mbio za riadha na baiskeli, Club House, na eneo maalum la kukusanyia taka.

Fursa za Uwekezaji

NHC imekusanya Sh.Bilioni 2.9 kutokana na mauzo ya nyumba katika mradi huo na mauzo yanaendelea kwa kasi, na wateja kutoka ndani na nje ya nchi wana hamu kubwa ya kuwekeza.

NHC inahamasisha Watanzania wote, wakiwemo waishio nje ya nchi (Diaspora), kuchangamkia fursa hiyo kwa kuwasiliana na ofisi za NHC.

Mradi wa 711 Kawe Residence ni kielelezo cha uwekezaji mkubwa na maendeleo ya kisasa yanayotekelezwa na NHC.

Ujenzi huo unatarajiwa kubadilisha kabisa mandhari ya Dar es Salaam na kutoa makazi bora kwa Watanzania.

Huu ni mfano wa jinsi Tanzania inavyoendelea mbele kwa kasi katika kuboresha miundombinu na kuboresha maisha ya wananchi wake.

Next Post
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira yapokea taarifa ya athari kwa Mazingira iliyotokana na mvua za El Nino

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira yapokea taarifa ya athari kwa Mazingira iliyotokana na mvua za El Nino

Tanzania kutumia Nyuklia kuzalisha umeme,mahitaji yanakua kwa asilimia 10 hadi 15 kwa mwaka

Tanzania kutumia Nyuklia kuzalisha umeme,mahitaji yanakua kwa asilimia 10 hadi 15 kwa mwaka

DCEA yamnasa wakala wa dawa za kulevya Tanzania,yumo bibi wa miaka 70

DCEA yamnasa wakala wa dawa za kulevya Tanzania,yumo bibi wa miaka 70

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:9
  • Today's page views 10
  • Total visitors 16,045
  • Total page views 18,204

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In