NA MWANDISHI WETU
TAASISI ya Hizb ut Tahrir / Tanzania imeungana na watanzania wengine kutoa mkono wa pole na kuifariji familia ya kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Muhammad Ali Kibao ambaye alitekwa Septemba 6, 2024 na kisha kuuwawa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Septemba 12,2024 na Mwakilishi wa vyombo vya habari wa taasisi hiyo Masoud Mselem amesema wao kama taasisi wanalaani vikali utekaji huo na mauaji hayo ya kikatili.
Mselem amesema vitendo vya utekaji vinavyopelekea kupotezwa au kuuliwa kikatili si vigeni nchini kwani, vimekuwapo kwa muda sasa, ambapo wapo wengine hawajuulikani walipo katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji mkoanji Pwani
‘’Matukio kama haya sio tu yanaleta hofu,ukosefu wa amani, kuchafuka na kuathirika haiba ya serikali, bali pia ni kielelezo cha wazi cha kukosekana uwajibikaji kwa kuwa dola ndio mdhamini mkuu na mlinzi wa usalama wa raia, mali zao na heshima zao.
‘’Matukio kama haya yanaonesha wazi wazi kushindwa kwa mfumo wa kibepari na demokrasia yake ulimwenguni kote, kwa kuwa mfumo huo unazua machafuko, vurugu na utovu wa amani kwa wanadamu’’amesema Mselem
Mselem ameongeza kuwa ni wazi, ulimwengu unahitaji mfumo wa haki na uadilifu wenye uwezo wa kudhamini ulinzi wa raia, maisha yao, mali zao na heshima zao.




Discussion about this post