• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

INEC yawaasa watendaji wake kuwa makini

by bajeti
September 14, 2024
in Habari
0
INEC yawaasa watendaji wake kuwa makini

Watendaji wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao ni Mratibu wa Uandikishaji wa Mkoa, Maafisa Waandikishaji, Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ugavi na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri kutoka Mkoa wa Dodoma wakila kiapo cha kujitoa uanachama na kile cha kutunza siri muda mfupi kabla ya kuanza mafunzo yao ya siku mbili kuhusu uboreshaji yaliyofanyika Makoa Makuu ya INEC jijini Dodoma Septemba 14, 2024. (Picha na INEC).

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewaasa watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kutekeleza majukumu yao kwa umakini  ikiwemo utunzaji wa vifaa vya uandikishaji.

Wito huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa uboreshaji wa Daftari ngazi  ya mkoa na halmashauri za Mkoa wa Dodoma Septemba 14, 2024.

“Vifaa hivi (vya uboreshaji wa Daftari) vimenunuliwa kwa gharama kubwa sana na vinatarajiwa kutumika katika maeneo mengine ya uandikishaji nchini. Kutokuwa makini katika utunzaji wa vifaa hivi kutapelekea athari kubwa katika ukamilishaji wa zoezi hili muhimu.,” amesema Jaji. Mbarouk wakati akisisitiza umuhimu wa kutunza vifaa hivyo”amesema Jaji Mstaafu Mbarouk

Amewataka watendaji hao kuzingatia maelekezo yote yatakayotolewa na Tume ili waweze kuyafanyia kazi wakati zoezi litakapokuwa limeanza.

Wakati huohuo, akifungua mafunzo kama hayo mkoani Singida, Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,Dkt. Zakia Mohamed Abubakar amesema matokeo bora ya zoezi la uboreshaji wa daftari yatatokana na matokeo bora ya zoezi hilo yanategemea uwepo wa ushirikiano mkubwa kati ya watendaji wote wa uboreshaji, serikali, vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi.

“Ninawasihi muwe na ushirikiano mzuri na wa karibu na Tume wakati wote mtakapokuwa mnatekeleza majukumu yenu na ikiwa mnahitaji ufafanuzi au maelekezo yeyote, msisite kuwasiliana na Tume,” amesema mjumbe huyo wa Tume.”amebainisha Dkt.Abubakar

Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya Mzunguko wa tano wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao utajumuisha Mkoa wa Dodoma katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Halmashauri za Wilaya ya Bahi, Chamwino na Kongwa, ambapo Mkoa wa Manyara katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu na Wilaya ya Kiteto na Simanjiro na Mkoa wa Singida.

Uboreshaji wa daftari kwenye maeneo hayo utaanza Septemba 25,2024 hadi  Oktoba 01, 2024 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni

 

Next Post
Polisi yachunguza kifo cha Daktari aliyekutwa amefariki

Polisi yachunguza kifo cha Daktari aliyekutwa amefariki

Russia yatishia kuligeuza Jiji la Kiev,Ukraine kuwa’’ lundo lililoyeyushwa’’

Russia yatishia kuligeuza Jiji la Kiev,Ukraine kuwa’’ lundo lililoyeyushwa’’

TFC yakabidhi tani 61,000 za mbolea ya rukuzu

TFC yakabidhi tani 61,000 za mbolea ya rukuzu

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In