NA MWANDISHI WETU,DODOMA
JESHI la Polisi kwa kushirikiana na wataalam wengine wa uchunguzi, linachunguza kifo cha Daktari Dismas Dominic (Chami 32), mkazi wa Ulyankulu aliyekuwa anafanya kazi katika Kituo cha Afya Ulyankulu ambaye amekutwa amefariki dunia huko katika eneo la Kombo Masai Kata ya Malolo Mkoa wa Tabora.
Kwa mujibu wa taarifa ya iliyotolewa Septemba 15,2024 na Msemaji wa Jeshi la Polisi jijini Dodoma DCP David Misime amesema mwili wake umekutwa ukiwa na dripu yenye dawa ambayo haijafahamika mkononi.
Amesema Daktari huyo alimuaga Mkuu wake wa kazi na mke wake Septemba 2,2024 kuwa, anaelekea Tabora kushughulikia akaunti yake ya benki iliyokuwa na changamoto na angelirejea Septemba 3,2024.
‘’Septemba 4,2024 hakupatikana kupitia mawasiliano yake ya simu. Septemba 10,2024 Daktari Mkuu wa Kituo hicho cha afya akiambatana na mke wa Dkt. Dismas Dominic (Chami) walifika katika kituo cha Polisi na kutoa taarifa ya kutokuonekana kwake toka Septemba 2,2024.
‘’Tarehe hiyo hiyo Dkt. Dismas Dominic (Chami) alimtumia ujumbe mke wake kwa njia ya Whatsapp unaosema
“Nisamehe sana baada ya dakika chache sitakuwa nanyi duniani,simamia kila kitu nilichoanzisha pesa zote zipo akaunti ya CRDB simamia na watoto wa some kwa heri”.amesema DCP Misime
DCP Misime ameongeza kuwa baada ya ujumbe huo hakupatikana tena hadi alipopatikana Septemba 13,2024 majira ya saa tatu usiku akiwa amefariki dunia
‘’Uchunguzi wa awali umebaini kuwa, alishajaribu kujiua mara mbili’’amebainisha DCP Misime




Discussion about this post