• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Friday, May 29, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

‘Mapapa’ wa biashara dawa za kulevya wahamia kwenye vyakula vinavyopendwa na watoto

Zimo jamu,asali,keki na biskuti,ni jukumu la kila mtanzania kupambana na ujangili huo

by bajeti
September 20, 2024
in Habari
0
DCEA yamnasa wakala wa dawa za kulevya Tanzania,yumo bibi wa miaka 70
Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

NI ‘ujangili wa afya ya binadamu’,hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya kubainika kwa baadhi bidhaa za vyakula vinavyopendwa na watoto kuwekwa dawa za kulevya.

Hatari hiyo inakuja wakati baadhi ya vyakula hivyo hununuliwa na wazazi wengi wa kipato cha chini  na vingine kama vyakula vya mara kwa mara katika jamii.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya ya Mwaka 2023 iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera,Bunge na Uratibu) na  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imeeleza kuwa matukio ya kuwepo kwa bidhaa za vyakula zinazotengenezwa kwa kutumia dawa za kulevya yameanza kushamiri hapa nchini.

Taarifa hiyo imefafanuwa kuwa kuanzia mwaka 2020,Mamlaka ilibaini na kukamata vyakula vilivyochanganywa na dawa za kulevya aina ya bangi katika matukio tofauti wakati wa utekelezaji wa operesheni zake.

‘’Vyakula vilivyobainika na kukamatwa ni pamoja na keki,biskuti,jamu na asali.

‘’Hali hii inaonesha kuwa tatizo hili linaendelea kuongezeka nchini na hasa ikizingatiwa  wafanyabishara hawa wenye nia ovu hutumia vyakula vinavyopendwa na watoto hivyo kuwaingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya bila kujua na hatimaye kuwa waraibu.

‘’Mwaka 2023 vyakula vyenye dawa za kulevya vilivyokamatwa ni paketi 17 za biskuti zenye uzito wa kilogram 2.04 zikihusisha watuhumiwa wanne wote wanaume.’’imeongeza taarifa hiyo

Hatari zaidi ya kuwa na kizazi chenye uraibu wa dawa za kulevya unakuja baada ya kuibuka uingizaji na matumizi ya dawa za kulevya aina bangi mpya inayoitwa ‘’skanka’’ ambayo inadhaniwa kuzalishwa nchi za Kusini mwa Afrika

Dawa hizo za kulevya aina ya skanka inadaiwa kuwa  na mchanganyiko wa aina mbalimbali za bangi kama Cannabis sativa na Cannabis indica huku ikiwa na kiasi kikubwa cha kemikali yenye sumu aina ya Tetrahydrocannabinol (THC) hivyo kuwa na athari kubwa zaidi kwa watumiaji.

Kemikali hiyo inadaiwa kuharibu mfumo wa fahamu,akili  na kusababisha magonjwa yasiyoambukizwa kama vile moyo,figo na kwamba matumizi ya skanka kwa wajawazito yanaweza kuathiri kwa mtoto aliye tumboni  kwa kuathiri maendeleo ya ubongo na kuzaliwa na uzito mdogo.

Septemba 10,2024 jijini Dar es Salaam Kamisha Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo alitoa taarifa ya kukamatwa kwa kiasi kikubwa cha dawa za kulevya aina skanka iliyofikia tani 1.8 ikiwa ni sawa na kilogramu 1,815

Kamishna Jenerali Lyimo amebanisha kuwa mmoja kati ya watuhumiwa waliokamatwa ni Richard Henry Mwanri mwenye umri wa miaka 47 mkazi wa Mbezi Makonde wilayani Kinondoni Mkoa wa  Dar es Salaam ambaye anadaiwa kuwa wakala wa kupokea dawa za kulevya kutoka nchi mbalimbali duniani na kisha kuziingiza nchini kwa usafiri wa magari zikiwa zimefichwa kwa kuchanganywa na bidhaa zingine na baadaye kuzisambaza kwa wauzaji wengine katika maeneo mbalimbali nchini.

Kamishna Jenerali Lyimo amebainisha kuwa kwa siku za hivi karibuni dawa za kulevya aina ya skanka zimekuwa zikikamatwa mara kwa mara nchini.

Hata hivyo ukamataji mkubwa wa dawa za kulevya unaofanyika nchini ni matokeo chanya ya uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanya na Serikali chini ya Uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye amedhihirisha dhamira ya kulinda kizazi cha sasa na kijacho kwa kuimarisha mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya

Licha ya majukumu ya DCEA ya Kudhibiti,Kupambana na Kukamata dawa za kulevya lakini kila mtanzania anawajibu wa kushiriki kikamilifu katika kusaidia mapambano haya kwa kuwa athari zake si kwa familia pekee bali kwa taifa zima.

Next Post
TFRA:Matumizi ya mbolea yafikia tani 840,000 mwaka 2023/2024

TFRA:Matumizi ya mbolea yafikia tani 840,000 mwaka 2023/2024

Upendo kwa watoto

Upendo kwa watoto

ACT-Wazalendo yaeleza mikakati yake kudhibiti biashara dawa za kulevya

ACT-Wazalendo yaeleza mikakati yake kudhibiti biashara dawa za kulevya

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:10
  • Today's page views 10
  • Total visitors 16,603
  • Total page views 18,841

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In