• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Rais Dkt. Samia aridhishwa na kasi ya Waziri Aweso katika miradi ya maji

avunja rekodi kasi ya upatikanaji wa maji,Visima 900 kuchimbwa nchini.

by bajeti
September 25, 2024
in Mazingira
0
Rais Dkt. Samia aridhishwa  na kasi ya Waziri Aweso katika  miradi ya maji

Mradi wa Maji wa Mtyangimbole wilayani Madaba Mkoa wa Ruvumaambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan aliweka jiwe la msingi Septemba 24,2024

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,RUVUMA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Wizara ya Maji kwa kusimamia na kuhakikisha lengo lililoainishwa  katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya kuwafikishia huduma ya maji Watanzania inafikiwa.

Pongezi hizo amezitoa Septemba 24,2024 wilayani Madaba  Mkoa wa Ruvuma wakati akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Mtyangimbole kwa niaba ya miradi mingine 30 inayoendelea mkoani humo.

Zoezi hilo la uwekaji wa jiwe la msingi lilienda sambamba na kupokea taarifa ya uchimbaji wa visima 900 vya maji nchini.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo,Rais Dkt.Samia amesema anaridhishwa na utendaji wa Wizara ya Maji inayosimamiwa na Waziri Jumaa Aweso pamoja na Katibu Mkuu Mhandisi Mwajuma Waziri kutokana na Maendeleo ya Sekta ya Maji ambayo sasa yanaonekana sehemu mbalimbali nchini.

Amesema Ilani ya CCM inaitaka wizara hiyo kuhakikisha inafikisha huduma ya maji kwa asilimia 85 vijijini na asilimia 95 mijini lakini mwenendo wa wizara unaonesha kuwa hadi kufikia mwaka 2025 huduma hiyo itakuwa imevuka malengo.

Aidha, Rais Dkt. Samia amemuagiza Waziri Aweso kuhakikisha mradi huo wa Mtyangimbole unakamilika ndani ya miezi mitatu ili wananchi wapate huduma ya majisafi na salama.

Kwa upande wake Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema utekelezaji wa miradi ya maji nchini unakwenda vizuri na kwamba wizara haitakuwa kikwazo katika kuhakikisha lengo la Serikali linafikiwa kwa wakati.

Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Maji Jumaa Aweso Septemba 24,2024 wilayani Madaba Mkoa wa Ruvuma wakati akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Mtyangimbole.

Akiwasilisha taarifa ya Mradi wa Maji wa Mtyangimbole pamoja na program ya uchimbaji wa visima 900, Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amesema hadi sasa utekelezaji wa programu hiyo inayokusudia kuchimba visima  vitano kwa kila jimbo la uchaguzi nchini umefanikiwa kukamilisha visima 254 huku visima vingine vikiendelea kuchimbwa sehemu mbalimbali nchini,

Next Post
Kuelekea Siku ya Mbolea Duniani:Mazingira wezeshi yawa chachu ukuaji Tasnia ya Mbolea

Kuelekea Siku ya Mbolea Duniani:Mazingira wezeshi yawa chachu ukuaji Tasnia ya Mbolea

Dkt.Biteko awataka wazazi na walimu kuwaandaa wanafunzi kuwa viongozi bora wa siku zijazo

Dkt.Biteko awataka wazazi na walimu kuwaandaa wanafunzi kuwa viongozi bora wa siku zijazo

Kuelekea Siku ya Mbolea Duniani, ni wakati mzuri wa kuelewa dhana ya matumizi sahihi ya mbolea

Kuelekea Siku ya Mbolea Duniani, ni wakati mzuri wa kuelewa dhana ya matumizi sahihi ya mbolea

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In