NA GOODLUCK HONGO
KONGAMANO la Kimataifa la kujadili Tasnia ya Mbolea nchini linatarajiwa kufanyika jijini Dodoma na kuwakutanisha zaidi ya washiriki 250 kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Kongamano hilo linaloelezewa kuwa la aina yake litafanyika Oktoba 11 na 12,2024 jijini humo kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mbolea Duniani inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo Oktoba 13.
Hayo yameelezwa Oktoba 1,2024 mkoani Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Joel Laurent wakati akizungumza na waandishi wa habari
Amesema kongamano hilo litawakutanisha pamoja wadau wa Tasnia ya Mbolea kitaifa na kimataifa na linatarajiwa kuja na majibu ya changamoto inayoikabilia tasnia hiyo na wakulima kwa ujumla
‘’Kongamano hilo litahidhuriwa na washiriki takribani 250 kutoka ndani na je ya nchi watakaojadili mada mbalimbali kuhusu Tasnia ya Mbolea kwa ujumla wake.
‘’Hii itatoa fursa kwa wadau hao kujadili kwa pamoja mabadiliko chanya ya Tasnia ya Mbolea,kubadilishana uzoefu na kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazoikabilia tasnia hiyo
‘’Mada zinakazojadiliwa ni pamoja na usimamizi na udhibiti wa mbolea,mchango wa afya ya udongo katika kuimarisha usalama wa chakula nchini ikiwemo matumizi ya Tehama katika kusimamia Tasnia ya Mbolea’’amesema Laurent
Laurent amefafanuwa kuwa wakati Kongamano hilo likiendelea ,mkoani Manyara maadhimisho hayo yataendelea kuanzia Oktoba 10,11 na 12,2024 na yatahusisha maonesho kutoka kwa wadau mbalimbali wa Sekta ya Kilimo
‘’Lengo la maadhimisho ya Siku ya Mbolea Duniani ni kupanua wigo wa kuelezea masuala mbalimbali katika tasnia hiyo ikiwemo mafanikio yake nchini,kutoa elimu kwa wadau,hususani wakulima na wafanyabiashara,na kauli mbiu kwa nwaka 2024 ni ‘’Tuongee Mbolea,Kilimo ni Mbolea
‘’Kauli mbiu hii inaenda mbamba na juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuthamini umuhimu wa mbolea katika Sekta ya Kilimo ambako kwa misimu mitatu mfululizo Serikali imeendelea kuwanufaisha wakulima kwa kuweka ruzuku kwenye mbolea’’ameongeza Laurent
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ruzuku Kitaifa Louis Kasera amesema hadi sasa zaidi ya wakulima Milioni nne wamesajiliwa katika mfumo wa ruzuku ya mbolea ambao umesaidia pia kuondoa mbolea feki.




Discussion about this post