• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

TFRA yanadi fursa Tasnia ya Mbolea Oman

by bajeti
October 1, 2024
in Habari
0
TFRA yanadi fursa Tasnia ya Mbolea Oman

Afisa Udhibiti Ubora Mkuu, Esther Kapakala wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) akizungumza na mwekezaji wa Kiwanda cha Mbolea aina ya NPK Fahad Ali Al Hajri wakati wa kongamano baina ya Tanzania na Oman kufunguliwa Septemba 29, 2024 nchini Oman.(Picha na TFRA)

Share on FacebookShare on Twitter

MUSCAT,OMAN

MAMLAKA ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) ni miongoni mwa taasisi zilizoshiriki katika Kongamano la Kibiashara baina ya Tanzania na Oman lenye lengo la kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uchumi baina ya nchi hizo mbili.

Kongamano hilo lililohusisha takribani watanzania 300 limefanyika  Septemba 29, 2024  jijini Muscut nchini Oman na kuibua wawekezaji katika nyanja mbalimbali ikiwemo tasnia ya mbolea.

Akizungumza katika kongamano hilo mgeni rasmi na Waziri wa Biashara, Viwanda na Uhamasishaji Uwekezaji wa Oman,Qais bin Mohamed Al Yousuf amesema, kumekuwa na ongezeko la asilimia 23.8 la kampuni za kitanzania zilizowekeza nchini Oman kutoka asilimia 13.5 ya kampuni zilizokuwa zimewekeza miaka miwili iliyopita.

Naye Balozi wa Tanzania nchini Oman,Fatma Rajab amezungumzia kuendelea kukua kwa ushirikiano baina ya nchi hizo na kueleza nia kubwa ni kuimarisha mashirikiano katika sekta za kilimo na nishati.

Akizungumza na mmoja wa wawekezaji mwenye kiwanda cha kuzalisha mbolea aina ya NPK,Fahad Ali Hajri, Afisa Udhibiti Ubora Mkuu kutoka TFRA, Esther Kapakala ameeleza, vigezo anavyotakiwa kuzingatia ili kufanya biashara ya mbolea nchini kuwa ni pamoja na  kusajili kampuni yake kwa kuzingatia vigezo vyote vya kusajili.

Aidha, Kapakala amemshauri mwekezaji huyo kufanya kazi na Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) kutokana na kampuni hiyo kuwa ni ya Serikali na kumhakikishia kuungwa mkono na shirika ili kufikia hatua njema ya kutimiza nia ya kufanya biashara ya mbolea nchini Tanzania.

Pamoja na hayo, amemwezesha mdau huyo kupata mawasiliano ya kampuni mbalimbali za mbolea ili kufanya mazungumzo nao yatakayomwezesha kuwa na uelewa na uamuzi wa kujihusisha na biashara hiyo nchini Tanzania.

Mwekezaji Fahad Hajri anazalisha mbolea aina za NPK zenye virutubisho vya 12:2:35+TE, 20:20:20+TE na mwisho ni 10:50:10+TE ambapo alielezwa mbolea hizo zitapaswa kusajiliwa kwanza endapo bado hazijasajiliwa nchini.

Akihitimisha mazungumzo baina yao, Kapakala ameeleza kuwa, Mamlaka ina jukumu la kuthibitisha ubora wa mbolea endapo unalingana na ule uliowasilishwa na mwekezaji wakati wa kuomba vibali vya kuingiza bidhaa hiyo nchini ili kuhakikisha wakulima wanapelekewa bidhaa zenye ubora

Next Post
Kongamano la Kimataifa kujadili Tasnia ya Mbolea kufanyika Dodoma

Kongamano la Kimataifa kujadili Tasnia ya Mbolea kufanyika Dodoma

Ushirikiano wa Tanzania na Falme za Kiarabu (UAE) wazidi kuimarika

Ushirikiano wa Tanzania na Falme za Kiarabu (UAE) wazidi kuimarika

Benki ya Dunia yaridhishwa utekelezaji miradi ya maji Pangani

Benki ya Dunia yaridhishwa utekelezaji miradi ya maji Pangani

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In