• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Kiruavunjo:wamshukuru Rais Dkt.Samia kuwapelekea miradi ya Majisafi na Usafi wa Mazingira

Benki ya Dunia waikagua na kuridhika na utekelezaji wake

by bajeti
October 3, 2024
in Mazingira
0
Kiruavunjo:wamshukuru Rais Dkt.Samia kuwapelekea miradi ya Majisafi na Usafi wa Mazingira

Wananchi wa Kiruavunjo wilayani Moshi Mkoa wa Kilimanjaro wakifurahia Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira utakaowawezesha kupata maji safi kwa asilimi 100.(Picha na mpigapicha wetu)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,KILIMANJARO

MIRADI ya Majisafi na Usafi wa Mazingira, pamoja na Chombo cha Watumia Maji imekaguliwa katika Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro ili kuona ubora wake kwa jamii.

Hilo limefanyika kwa wataalamu wa Sekta ya Maji na wawakilishi wa Benki ya Dunia kukagua Mradi wa Uboreshaji Huduma ya Maji Kiruavunjo Kusini na Mradi wa Usafi wa Mazingira katika Zahanati ya  Kikalala .

Mradi huo wa Uboreshaji Huduma ya Maji Kiruavunjo Kusini unahudumia wakazi zaidi ya 6000  na kukamilika kwake kutaongeza  hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa asilimia 100.

Aidha, pamoja na hilo lakini pia ukaguzi umefanyika katika Chombo cha Watumia Maji  cha Kiruakahe kinachohudumia vijiji 28, ili kuona namna wanavyoweza kutoa huduma kwa wananchi.

Kwa upande wa eneo la Usafi wa Mazingira ukaguzi umefanyika katika Zahanati ya Kikalala ambayo ilipata fedha kwa ajili ya kutengeneza miundombinu ya usafi wa mazingira kiasi cha Sh.Milioni 470.

Mradi wa Usafi wa Mazingira Kikalala umewezesha wakazi wa eneo hilo kuwa na uhakika wa huduma bora za afya na usalama dhidi ya magonjwa yanayosababishwa  na uchafu.

Meneja wa Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) ,Mhandisi Musa Msangi akizungumza akitoa maelezo juu ya maendeleo ya Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira wa Kiruavunjo wilayani Moshi Mkoa wa Kilimanjaro Oktoba 2,2024

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo Oktoba 2,2024 katika eneo la mradi huo Kiruavunjo,Meneja wa Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro Mhandisi Mussa Msangi amesema kwa sasa wananchi wanapata maji kwa asilimia 45 na pindi mradi ukikamilika huduma ya maji itakuwa asilimia 100.

‘’Leo tumetembelea na kujionea mradi huu na chombo cha watumiaji maji,chombo imara imara kinachohudumia vijiji 28 na awali tulikuwa na upungufu wa maji lakini sasa wanatumia maji kwa sababu mradi umefika asilimia 80.

‘’Ndani ya mwezi huu wa 10,2024 wataanza kuongeza maji kiasi cha lita 500020 na walikuwa wanakusanya mapato ya kiasi cha Sh.Milioni 6 na yataongezeka hadi Sh.Milioni 10 na kufanya jumla ya mapato wanayopata kama Jumuiya ya Sh.Milioni 60 kwa mwezi  na yatafikia Sh.Milioni 63.

‘’Haya ni mafanikio makubwa sana na itaongeza huduma ya upatikanaji wa maji na watu 15,000 watumiaji wa maji katika wilaya yetu na kutusukuma kutoka asilimia 84.5 hadi asilimia 90.2 itakapofika mwezi Juni 2025’’amesema Mhandisi Msangi

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro Dkt.Juma Mapokaleo kitoa maelezo juu ya Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira ulivyosaidia Zahanati ya Kisalala kwenye ujenzi wa vyoo ili kuboresha afya za wagonjwa wanaohudumiwa katika eneo hilo

Akizungumzia kuhusu Mradi wa Zahanati ya Kisalala,Mganga Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro Dkt.Juma Mapokaleo amesema walipokea fedha za mwaka wa fedha 2023/24 kwa ajili ya kutengeneza miundombinu ya Usafi wa Mazingira

‘’Kwa kutekeleza mradi huu tunapata faida ya kuhakikisha taka zote zinazozalishwa kwenye Zahanati zinaweza kuchomwa na kuteketezwa kabisa lakini inazidi kutupa hamasa kwa wananchi ambao  tunaowahudumia katika eneo hili kuwa tunatakiwa kujitunza kwa usafi

‘’Baada ya kuwa na vyoo bora na sehemu za kunawia mikono,kabla ya kuanza huduma zetu asubuhi  tunawapa elimu ya afya pamoja na kuwasisitiza namna bora ya kutumia miundombinu ya maji safi ili kuweza kujikinga ya magonjwa ya mlipuko na mengine’’amesema Dkt Mapokaleo

Naye mkazi wa Kiruavunjo Hellen Msofe amesema wamefurahi kupata mradi huo wa maji safi kwa kuwa awali walikuwa wakitumia maji ya mtiririko na kusababisha athari za maradhi ya tumbo na kupata matatizo kwa muda mrefu

‘’Lakini kwa sababu Mama Samia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameona kuna umuhimu wa kutusaidia sisi akina mama tunaoishi maeneo haya kwa kutuletea mradi mkubwa wa maji kama huu’’amesema Msofe

Next Post
Kamishna Jenerali Lyimo:Tutavunja mitandao yote mikubwa ya dawa za kulevya

Sababu waraibu dawa za kulevya kuharibika sura ‘kulala wakiwa wamesimama’

IGP Wambura atembelea Kigoma kuangalia hali ya usalama

IGP Wambura atembelea Kigoma kuangalia hali ya usalama

Kuelekea Siku ya Mbolea Duniani,TFRA yataja mafanikio ya kampeni ya ‘Kilimo ni Mbolea’

Kuelekea Siku ya Mbolea Duniani,TFRA yataja mafanikio ya kampeni ya ‘Kilimo ni Mbolea’

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:6
  • Today's page views 6
  • Total visitors 13,062
  • Total page views 14,807

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In